Namleta kwenu Laudit Mavugo

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
-Huyu strika tishio kwa mabeki wale visiki alizaliwa miaka 25 iliyopita, nchini Burundi.. a.k.a yake ni Tormentor.

-Mwaka 2011 kocha wa Police FC ya Rwanda, "Mtalamu" Goran Kopunovic aligundua kipaji cha ajabu cha huyu kijana na kuamua kumsajili.. akiwa na miaka 21 tu!

-Msimu wa kwanza tu, alifunga goli 12 [maajabu yaliyoje!!] na timu yake ikakamata nafasi ya 2 katka ligi kuu nyuma ya APR.

-Kutokana na kuonesha kiwango kikubwa saana.. akawa bidhaa adimu nchini Rwanda.. Hii ilisababisha apite katika timu kama AS Kigali na Kiyovu FC.

-Mwaka 2014 matajiri wa Burundi [Vital'O] walipata habari zake, nao wakapanda dau na kumsajili.. Katika msimu wake wa kwanza tu alitupia goli 29 katka mechi 28 [what a player?!] na kuiewezesha kuchukua ubingwa wa ligi.

-Baada ya ligi kuisha, Simba SC nayo imempandia dau ili aitumikie kwa misimu miwili ijayo.. Hii ni kutokana na shughuli yake uwanjani.


Maoni Yangu: "Baada ya kupita miaka mingi tukisubiri striker wa maana.. hatimae amefika, naye ni Laudit Mavugo."
- sembo





 
Last edited by a moderator:
Hamis Tambwe

Dan Serunkuma
 
Usajili wa vyombo vya habari kama kawaida ya mikia. Ngoja ndondo zianze kama hamjamfukuza kabla ya ligi
 
Hamis Tambwe

Dan Serunkuma

Msimu wa kwanza Tambwe unajua alichofanya.. msimu uliofata alishndwa kuendana na mfumo wa kocha mpya.. na ndo mana akatemwa ili aache nafasi kwa mtalamu Kiongera, ambaye naye bahati mbaya aliumia.

Dan alishindwa kuendana na kasi ya Simba SC.. ndo maana akaomba mwenyewe kuondoka.. huyu HATUKUMUACHA.

Naamini kama Mavugo alifunga goli 12 msimu wake wa kwanza nchini Rwanda.. akafunga goli 29 msimu wake wa kwanza nchini Burundi.. kwanini asifunge goli 20+ msimu wake wa kwanza Bongo??

Japo mda utaongea, naimani kubwa na The Burundian Tormentor Mavugo.
 
Usajili wa vyombo vya habari kama kawaida ya mikia. Ngoja ndondo zianze kama hamjamfukuza kabla ya ligi

Haha.. Sasa tutamfukuzaje kabla ya ligi kuanza?
 
Mkuu, hakuna picha zake au walau kipande cha video?
 
Mkuu, hakuna picha zake au walau kipande cha video?

Mkuu natumia kisimu cha tochi hivyo ku upload inakua ngumu.. Lakini ukiingia google au Youtube utakutana na maajabu ayafanyayo.
 
Striker mpya Simba SC aja na rekodi za Ronaldo na Messi!!

Laudit Mavugo amekuja na rekodi ya kuwa na uwiano wa goli moja au zaidi katika mechi moja katika ligi kuu.

Katika msimu uliopita wachezaji waliokua na uwiano huo ni Christiano Ronaldo [CR7], Messi na "Tormentor" Laudit Mavugo.

CR7 alicheza mechi 38 akafunga goli 48, uwiano wake ni 1.4!

Messi alicheza mechi 38 akafunga goli 43, uwiano wake ni 1.2!

Laudit Mavugo alicheza mechi 28 akafunga goli 29, uwiano wake ni 1.04!
 

Tambwe alishindwa kufuata mfumo wa kocha gani?

Toa sababu Dan ashindwe kuendana na kasi,ya Simba .Wakati mnamfukuza Tambwe na kumleta hamkujua hayo yote.Unanikumbusha kuna mwenzenu anaitwa Revocatus Kashaga,alikuwa anaanzisha mada kama zako siku hizi kaamua kuhamia kwenye siasa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu natumia kisimu cha tochi hivyo ku upload inakua ngumu.. Lakini ukiingia google au Youtube utakutana na maajabu ayafanyayo.
 
Last edited by a moderator:
Tambwe alishindwa kufuata mfumo wa kocha gani?

Toa sababu Dan ashindwe kuendana na kasi,ya Simba .Wakati mnamfukuza Tambwe na kumleta hamkujua hayo yote.

-Tambwe alishindwa kuendana na mfumo wa Phiri, ambaye alikua akimtaka ashuke chini kutafuta mipira kitu ambacho hakukiweza.. tofauti na kocha aliyetimuliwa aliyekua akimtaka akae katka 18 na kusubiri aletewe mipira, then yeye atupie kambani.

-Tanzania hatuna utaratbu wa kumpima mchezaji tunapomsajili.. Kiongera alikuja mgojwa, katika gemu ya kwanza akatoneshwa.. ila sasa yuko fiti, mjiandae kukutana na dhahama lake.

-Tatizo la Dan, ni kua alikua akicheza kama winga wa kushoto alipokua Gor Mahia na ndo namba anayokua comfortable.. sasa kaja msimbazi kocha anamchezesha mara 9 mara 10.. unategemea nini?.. pia hakua confortable na mazngra ya Simba SC, alipokua Gor Mahia, Dan alikua mfalme tena mfalme haswa.. sasa kaja huku kakuta kuna Mfalme Okwi, unategemea nini?? Lazima aombe POO.
 

Unajua Phiri alifukuzwa miezi mingapi baada ya Tambwe kuuzwa? Danny ambaye anaweza kurudi nyuma mbona nae alipigwa bench,na Why mumsajil mfalme wakati mnae mfalme Okwi?
 
Unajua Phiri alifukuzwa miezi mingapi baada ya Tambwe kuuzwa? Danny ambaye anaweza kurudi nyuma mbona nae alipigwa bench,na Why mumsajil mfalme wakati mnae mfalme Okwi?

-Phiri na Tambwe wote waliondoka katika dirisha dogo la usajili, i mean baada ya mtani jembe.

-Dan hatukumsajili ili aje awe Mfalme mpya, tulimleteta aje acheze mpira.. Yeye akataka kuleta ufalme wa Gor Mahia.

-Kuhusu Dan kupigwa benchi nishakuambia ni kwa sababu namba alizotaka kupangwa, zilikua zina wenyewe.. na si suala la kushuka chini na kuchukua mipira.
 

Very interesting,Phiri alimkataa Tambwe hafit kwenye mfumo wake then Phiri na Tambwe wote waliondolewa dirisha dogo .Hii akili au matope?
 
Hapa ndo huwa nakereka na soka la Bongo,
Ingekuwa ushindi ni mdomo tungekuwa tumeshachukua makombe ya dunia hata 10
 
Sembo Na simba yake anaivyoipamba!!

Ikianza ligi hapa hatutaki visingizio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…