Namna gani naweza kukadiria faida ya duka?

Namna gani naweza kukadiria faida ya duka?

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Habari ya leo wanajf!

Nina imani mko salama salimini! Ninaomba mnisaidie namna nzuri ya kuijua faida ya kwenye duka! Ninaomba mfikirie pia hali hii kuwa vitu ndani ya duka kila kimoja kina faida tofauti na kingine na huisha dukani tofauti na kingine.

Msaada tafadhali
 
Habari ya leo wanaJF,

Nina imani mko salama salimini!Ninaomba mnisaidie namna nzuri ya kuijua faida ya kwenye duka!

Ninaomba mfikirie pia hali hii kuwa vitu ndani ya duka kila kimoja kina faida tofauti na kingine na huisha dukani tofauti na kingine

Msaada tafadhali
 
Muuzaji wa kilo moja ya mchele, vocha ya mia tano,, pipi, biscuits moja, unga kilo moja, mafuta ya vibaba vya mia mia 🤔🤔🤔🤔
Duka la reja reja hata duka la vipodozi ni linaweza likawa la reja reja,duka la vifaa vya simu, vya ujenzi ,pikipiki nk linaweza likawa la reja reja.
 
Mbona simple tu, bei uliyonunua toa uliyouza mfano crate ya coca bei ya jumla 13,300 gawanya kwa 24 utapata 554.16 ukiuza moja ni 700 toa 550 utapata 150 ndio faida, rudia kwa kila bidhaa uliyouza hapo inabidi uwe na daftari
 
kua makini usidokoe faida hata mia ukifanya mchezo utambulia mshahara wa kufuta vumbi kwenye mashelfu mwisho wa mwezi na biashara haitakua
 
Kisha jumlisha zote tafuta profit in percentage mfano ukipata 10% ukiuza laki faid yako roughly ni 10,000
 
Vitu vingi kwenye biashara ya duka la rejareja vina faida kati ya 10%-20%,hivyo ukiuza mfano laki moja hapo faida ya uhakika ni elfu 10....labda kma unauza na pombe kali ndo zina faida kidogo!
Cha msingi uwe na daftari la mahesabu ya kila bidhaa unayouza!
 
Back
Top Bottom