Namna gani naweza kukadiria faida ya duka?

Ninauza vocha za simu,juisi za watoto,Mchele wa kupima,Katanga za kukaanga, mafuta ya kula,soda,mafuta ya kupaka,chumvi,sabuni yaani ni la mahitaji ya nyumbani!Ni kama duka-genge!
Duka la Mangi...kuli manage ni upate Muuzaji muaminifu au ukae mwenyewe la sivyo maji utaita Mma
 
Orodhesha vitu vyote na bei zake za manunuzi mbele yake weka bei ya kuuza mbele Tena weka tofauti kati ya bei yakuuzia hii tofauti ya kati ya bei ya kuuza na kununullia Ndiyo inaitwa faida ya kuuza bidhaa ukiijumlisha yote itakuletea faida ya jumla ya kuuza, faida ya duka utaipata baada kutoa matumizi ya kilasiku kma hujaelewa uliza
 
My friend km hujui hesabu iyo biashara soon utaifunga mganga mkuu wa kibiashara ni Hesabu hesabu hesabu. Inatakiwa kila bidhaa ujui hesabu yake umenunua ngap unauza ngap na imebaki ngap unaweza kuta mauzo ya laki hujapata ata 100 kwa vile no hesabu, yaani kiufupi before kuuza chochote unatakiwa ujue faida tayar vinginevyo utawalaumu TRA au utawalaumu waganga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…