Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
Hahaha..nachopenda kutoka watu wanaotoka katika jamii moja hapa dar ni kushirikiana kwao. Pale mabibo kuna wamasai wengi wengi sasa ukipita mida ya usiku kama hii pale nyuma cha chuo cha NIT utawakuta weeengi wamekaa kwenye majani chini ya miti wanajadili mambo yao.Kuna kijiwe flan maeneo ya temeke walikuwa wanakutana wanaouza kahawa na wale waaouza karanga kuandaa bidhaa.
Wakati hawa wanaandaa kashata na kuchemsha kahawa wengine wanachemsha karanga,sasa sikilizia kilugha kinavyogongwa hapo ni hatari.
Kwa mara ya kwanza ndio niliona namna kashata zinavyoandaliwa.
Inavutia sana kuishi lwa namna hii.