Namna pekee ya kuzuia Corona virus kusambaa

Namna pekee ya kuzuia Corona virus kusambaa

Masharti ya UKIMWI yalikua madogo sana.
1. Epuka ngono
2. Ama uwe na mpenzi mmoja mwaminifu na
3. Ukishindwa kabisa tumia kondom.
VERY SIMPLE bado watu walipukutika kwa starehe ya dakika tano tuh.
MASHARTI YA KIPINDUPINDU NDIO MADOGO ZAIDI
1. Epuka uchafu
2. Uwe msafi
3. Kula visafi
SASA HII
1. Epuka misongamano
2. Vaa mask
3. Usiwasalimie jirani
4. Unawe
5. Unywe maji
6. Usukutue na maji chumvi
7. Ukae nyumbani tu
8. Bar, sokoni, mpirani, kilabuni etc marufuku
9. Usisafiri
N.k
Niambie mtanzania na kunawa mikono wapi na wapi.
Kuvaa kondom tu tena zilitolewa bure na ikiuzwa ni mia watu wamekufa. Itakua sabuni, sanitaiza, maski nk?
Nini kifanyike!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini mbona nchi walizofungia watu ndani ndio zinaongoza kwa vifo?
 
M
Sisi tumemuachia Mungu.😃

Tukisema tuweke lockdown nchi nzima tutakufa kwa njaa kuliko hata COVID-19 yenyewe.

Mkuu haka slogan ka kufa njaa kanaletwa na nini? Hungary amekata ruzuku ya vyama vya siasa kwa 60% kwa Corona emergency.

Sisi tunaweza haya:

1. Kutoa support kwa wale watakao hitaji support kweli kweli.
2. 100% ya ruzuku ya vyama like kuchangia kutoa hiyo support kwa #1.
3. Hizi issue za bunge tuahirishe pesa ziende kwenye hiyo #1
4. Budget ya uchaguzi mkuu iende kwenye #1.
5. Miradi mikubwa yote kwa sasa isimame kuhakikisha hatutetereki kwenye #1.
6. Tuweke mfuko wazi kwa wasamaria wema ndani na nje kuchangia kwa akili ya #1.
7. Nk nk

Kwa hali ya sasa takwimu zingehuishwa tuachane na hii ficha ficha. Unaweza kuta labda hata miji ya kuanzia hiyo lockdown si yote. Labda ikawa ni 10% ya nchi.

Tusijikatie tamaa ya maisha hivyo. Tufe tukipigana siyo tufe tukisubiria.
 
Lakini mbona nchi walizofungia watu ndani ndio zinaongoza kwa vifo?
Hili pia linatafakarisha.
Ila napata picha wasingefungia hali ingekuwaje. Si ingekuwa mbaya zaidi shangazi, hata mara 10 ya ilivyo sasa.
 
Lakini hayo ni maoni yako tu, sio lazima uwe ukweli
Sasa shangazi ndio sio lazima iwe ukweli.
Lakini si kwa akili tu ya kawaida tu unapata picha.


(Halafu hiyo avatar hiyo ndoa ndio zile za kuchaguliwa na wazazi😃😃)
 
Hili pia linatafakarisha.
Ila napata picha wasingefungia hali ingekuwaje. Si ingekuwa mbaya zaidi shangazi, hata mara 10 ya ilivyo sasa.

Kuongezeka kwa maambukizi sehemu zenye lockdown imeelezwa vizuri kwenye bandiko la WEF.

Inapoelekea kwenye mafanikio vifo na cases hupanda hadi ikishafika peak kutokea hapo husika kuelekea katika hali iliyodhibitika.

Usichoke pitia chapisho la WEF vizuri.
 
Balaa hili nachokiona marekani atashilia usukani kwenye vifo ni swala la muda tu
 
Mmh kumbe, hadi Marekani? Mbona wao walichukua hatua haraka sana

Marekani walichelewa sana. Trump a sana. Alikaidi maonyo yote kuanzia kabla ya ugonjwa kuingia na hata baada ya ugonjwa kuingia USA.

Hali ya alivyofanya Trump kujali sana uchumi kuliko athari kwa maisha ya binadamu haina tofauti sana na sisi.

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums

Tofauti yetu sisi na Trump kwa sasa ni kuwa sisi tungali tunaendelea kupuuza maonyo yote.

Kimsingi tungali tunacheza bado na moto.
 
Sisi tumemuachia Mungu.😃

Tukisema tuweke lockdown nchi nzima tutakufa kwa njaa kuliko hata COVID-19 yenyewe.

Tungeweza anzia lockdown angalau dar na Zanzibar na sehemu zingine ambako tayari tuna wagonjwa na walioko kwenye quarantine.

Kufa njaa ni hoja dhoofu. Mbona kama nchi tuna raslimali nyingi?
 
Sweden na Japan hakuna total lockdown,lakini hizi nchi hazijaathirika Sana na huu ugonjwa,..

watu wanapeta mitaani Kama kawaida,Shule hazijafungwa nk

Maisha yanaendelea...
 
Maisha yetu yenyewe ni Total lockdown sa unataka tena tuongeze na lock ya corona....
Bora tuwe na lock moja tu...
kuna kipindi hapo kati HIV aliua sana lakini hatukuchukua maamuzi ya kila mtu kumpiga kufuri la chuma sehemu za siri halafu funguo tuzipeleke kwa mjumbe wa nyumba kumi.
 
Sweden na Japan hakuna total lockdown,lakini hizi nchi hazijaathirika Sana na huu ugonjwa,..

watu wanapeta mitaani Kama kawaida,Shule hazijafungwa nk

Maisha yanaendelea...

Mkuu hizo nchi unazozitaja hazina misongamano kama unayoiona masokoni, kwenye madaladala, ibadani nk kama makwetu.

Hawa pia wamechukua hatua mapema sana kabla ya gonjwa kulipuka vilivyo.

Hata hivyo Japan hawa hapa:

Japan's coronavirus containment strategy faces breaking point

Sweden nao wana visa si chini ya 4000 na vifo mia kidogo ndiyo kudunda huko?:

Sweden response to coronavirus outbreak divides opinion

Mkuu ingependeza zaidi mkaonyesha namna ya kuuvunja mnyororo wa maambukizi ya ugonjwa huu kabla hali haijawa mbaya zaidi.
 
Back
Top Bottom