Mkuu nimesoma vyema bandiko lako ambalo napenda nami nikujibu kwa nia njema kama ulivyoandika.
Kwanza nini maana ya lockdown. Lockdown si kuwafungia watu ndani bali ni kuwataka watu kubakia majumbani ili kuwatambua wenye maambukizi na waliohusiana nao ili kuwatenga. Katika lockdown hulazimishwi kukaa chumbani bali hata kutembea tembea around nyumbani kwako ni sawa. Ila si kukata mitaa.
Mfano wewe katika familia yako ukigundulika kuwa tu kuwa umegundulika kuwa na maambukizi, utachukuliwa kupelekwa sehemu maalum ambako pia tiba katika uangalizi itaanza mara moja. Wale uliokuwa nao watawekwa quarantine kwenye uangalizi kutambua kama nao tayari wameambukizwa na ili wasiambukize wengine.
Si wewe wala hawa uliokuwa nao watakakuwa tena na nafasi ya kuambukiza watu wengine zaidi. Mnyororo wako wa maambukizi utakuwa umevunjika na kuishia hapo. Hii ni hatua njema sana ya kuanza kuudhibiti ugonjwa huu. Kwani ndani ya siku 14 wenzio nao watathibitika kuwa na maambukizi au la.
Hapa tatizo wala si hofu. Anayeua wagonjwa kwa mamia kwa siku USA, Spain, Italy, UK nk si hofu ni Corona.
Tusidanganyane kwenye hili.
Tatizo la Corona ni tatizo kubwa sana ambalo kimsingi halijawahi kutokea tangia Vita 2 vya dunia vimalizike 1945.
Kwa hakika tatizo la ukubwa kama huu kwa akili yoyote ya kibinadamu haliwezi kuwa na utatuzi rahisi. Kwa yeyote anayependekeza ufumbuzi rahisi itakuwa ni kwa sababu ya kushindwa tu kuelewa sawa sawa, kuwa hali iko vipi.
Kuhusiana na bibi yako. Umkumbuke babu wa Loliondo. Alikuja moto akaishia zake baridi. Bibi yako anayejidhania fundi asijaribu kuonana na mgonjwa hata mmoja wa Corona akiwa haja niga zana kamili na maalum za kujilinda na magonjwa ya maambukizi kama haya.
Vinginevyo yeye mwenyewe atakuwa hatarini mno kuambukizwa.
Huu ugonjwa ni mbaya tena zaidi kwa wanaoitwa kina babu na kina bibi. Utakuwa umemtendea haki mno kumpa hilo angalizo.
Tusiogope lockdown badala yake tuone tunaielewa na jinsi gani tunaweza kujipanga kuipita salama:
Rwandan cabinet, PSs forfeit April salaries over coronavirus
Covid-19: Uhuru bans movement in and out of Nairobi
Kwa umoja wetu vita hivi tutavishinda.
Hata hivyo maslahi yetu kama taifa lazima yaje mbele kabla ya yale ya kibinafsi. Hapo mbona hata wa kuunga mkono juhudi watapatikana?
Kiufupi njia zote ngumu.
LockDown ni ngumu na yenyewe pia haitafanya maambukizi kukoma.
Maana wakati una LockDown utambue kuwa kuna wenye maambukizi umewafungia ndani pia. Yaani mimi nitamwambukiza na baba na mama kaka wadogo zangu bibi pia babu usisahau shangazi mjomba maana hapa tz nyingi ni familia pana na sio single famili.
Na utambue kuwa mimi ndiye mtafutiaji wa hii familia..
Kiufupi mimi kama mimi siliungi mkono la LockDown wala siliungi mkono la kunawa maji na sabuni.
Mbinu yangu mimi iko hivi:-
Hii ni njia laisi na nyepesi kuwahi tokea duniani kote.
Kikubwa kinachotuathiri BINADAMU ni hofu.
Kwahiyo kitu cha kwanza kufanya ni kuondoa HOFU.
Yaondolewe matangazo yote kwa televisheni juu ya waathirika na hata matangazo pia yatupwa kule.
Ichukuliwe kama mafua mengine.
Kitu cha pili,
Watafutwe waganga wa mitishamba/wakienyeji maana kwa madawa ya kizungu lazima tutachemsha.
Mimi binafsi nina bibi yangu nilimsikia akisema kuwa ikitokea nikampata mgonjwa mmoja basi nimpeleke kwanza kilingeni kwake wenda akafaulu.
Ni hayo tu kwa leo