SEHEMU YA SABA
Sauti ile ilikuwa kama ya mzee ambaye ilionyesha kabisa alikuwa amekabwa na kitu kooni,baada ya kuongea lugha na matashi yasioeleweka kwetu,ile sauti ilipokoma,mwanamke wa yule mtaalamu alikuja kutuita akasema jamaa anasema tuingie ndani.Tulipoingia kwenye chumba alichokuwepo huyo mtaalamu tulikuta chini kumetandikwa shuka jekundu na kumewashwa udi za kutosha,pia kulikuwa na chupa za bia za kutosha yaani unaweza sema kile chumba ilikuwa ni stoo ya kuhifadhia chupa za pombe.
Basi bhana tukafika tukaambiwa tukae chini ya lile shuka jekundu,sasa yule mtaalamu akachukua unga mweupe uliokuwa kama poda akaanza kutupaka usoni pamoja na mikononi,baada ya kutupaka akachukua kisosi cha udongo akaweka dawa moja iliyokuwa nyeusi kisha akaanza kusema.
Yeye "Mmekuya....naona mmekuya"
Aliendelea "Hapa mtapata mambo yenu ya kwende mzuri!"
Aliendelea "Naomba msiwe na hofu"
Kuna maneno mengine ambayo tulikuwa hatufahamu kamaanisha kitu gani,Jentre ndiye akawa anatutafsiria.Baada ya kupiga manyanga yake na kujiongelesha lugha tusizozifahamu,akaanza kutuambia mambo yafuatayo.
Yeye "Milimo ya bankoko elobaka boye,memela ngai deukshi litambala pona mwasi na ngai"
Yeye "Milimo ya bankoko elobaka boye,memela ngai troisi Khanga pona mwasi na ngai"
Jentre "Anasema,mizimu ya mababu imemwambia mumletee shuka mbili ya kujifunika kwa ajili ya mke wake"
Aliendelea "Pia anasema mizimu ya mababu zake imewataka mumletee vitenge pea tatu kwa ajili ya mke wake"
Yeye "Soki osali bongo,makambo ekozala malamu"
Jentre "Anasema,mkifanya hivyo walivyosena wazee mambo yenu yatakuwa mazuri!"
Kamugisha "Sawa sisi tumekuelewa,mimi nataka mambo yawe mazuri zaidi,Je tunaweza kumnunulia mke wake na vitu vingine kama zawadi?"
Mimi niliendelea kumtazama Kamugisha alivyokuwa na ujasiri wa kusema akamnunulie yule mke wa jamaa zawadi wakati hata mafanikio yenyewe hatujayaona.
Yeye " Nalingaka yo mingi mpe okozala na elonga mingi,bilimu bikosepela mpe mwasi na ngai mpe akosepela"
Jentre " Anasema,Wewe amekupenda sana na utafanikiwa sana,mizimu itafurahi na mke wake pia atafurahi"
Baada ya kuonekana tutakuwa watu wa mafanikio,alituambia usiku huo turudi tukapunzike halafu asubuhi hizo zawadi za mke wake zinunuliwe ili itakapofika jioni twende kuianza kazi ya kuyatafuta mafanikio yenyewe;Kwakuwa Kamugisha alikuwa amebaki kidogo na pesa za Kikongo tuliona siku iliyofuata tuondoke turudi pale Moba ili tukabadirishe angalau Dola 100 kwa ajili ya matumizi na mahitaji hayo.
Kabla ya kushuka Moba Kamugisha aliwasiliana na Jentre na kumueleza tulipokuwa tunaelekea na Jentre akamshauri hatuna haja ya kwenda huko kote na wakati hapohapo Kirungu kulikuwa kuna mtanzania aliyekuwa na duka la kuuza magodoro huwa anabadiri pesa,kwakuwa jamaa alisema ni mtanzania basi tukaona ni heri tukamuungishe mtanzania mwenzetu kuliko kushuka Moba.
Jentre alikuja akatupeleka hadi kwenye lile duka la mtanzania na bahati nzuri tulimkuta.
Kamugisha "Mambo vp kaka"
Mtanzania " Shwari ndugu zangu,nyie wabongo nini!"
Sisi "Eeeh!"
Mtanzania "Kiswahili tu namna tunavyoongea ndicho kinawatambulisha waswahili huku"
Aliendelea "Karibuni"
Kamugisha "Tulikuwa tunahitaji kubadili dollar 100 kaka"
Mtanzania "Hakuna tatizo karibuni sana"
Aliendelea "Mmekuja kuangalia fursa za kibiashara nini ndugu zangu!"
Kamugisha "Aaah hapana tumekuja kutembea tu na kubadili upepo!"
Mtanzania "Aaaah Kaka,haya bhana"
Aliendelea "Nilitaka kama mmekuja kuangalia fursa mnishirikishe nitawasaidia,mimi hapa ni mwenyeji huu ni mwaka wa 14 napambana hapa"
Kamugisha "Mazingira ya kibiashara yakoje hapa?"
Mtanzania "Ndugu zangu huku kuna hela ila sema tatizo haya makongomani yanapenda sana hela,kuna usumbufu mdogo mdogo kwa wapenda hela ila kuhusu hela hapa ipo,unajua bidhaa nyingi zinatoka Tanzania kwa njia ya maji kwasababu huku mabarabara hakuna"
Aliendelea "Hivyo kama ukiamua kuwekeza nyie njooni mpambane,pesa ipo!"
Kamugisha "Sawa kaka ila kwakuwa wewe ni mbongo mwenzetu sisi tulikuwa tumekuja kwa mtaalamu kwa ajili tu ya mambo yangu ya kazini"
Sasa jamaa alimwambia yule mtanzania japo kwa kumficha lakini alimueleza,mimi sikutaka kabisa jamaa amueleze mambo yetu na nilitaka iwe siri lakini jamaa akaamua kufunguka,japo hakumwambia kilichotupeleka ni kitu gani yeye alimwambia alienda kwa ajili ya mambo ya kazini kwake.
Mtanzania "Kuweni makini tu huku watanzania huwa wanajifanya wajuaji na wanatapeliwa sana"
Kamugisha "Kweli eeeh!"
Mtanzania "Siwadanganyi,nyie ni ndugu zangu ni lazima niwatahadharishe"
Aliendelea "Kwani mmefikia wapi?"
Kamugisha "Tulifikia Guest moja ipo kule chini ila kwasasa tunalala kwa ndugu yake mtaalamu"
Mtanzania "Wakati mnakuja nimewaona na jamaa mmoja mmeongozana nae,mnafahamiana nae?"
Kamugisha "Yes,jamaa tumekutana nae pale Kirando"
Mtanzania "Kwahiyo siku hizi yupo Kirando!"
Kamugisha "Unamfahamu mshikaji"
Mtanzania "Jamaa alikuwa fundi simu alipoona nadhani mambo hayaendi sawa akabadili upepo"
Kamugisha "Alikuwa fundi simu?,Mbona jamaa kwasasa ni mtaalamu na anafahamika sana pale Kirando!"
Mtanzania "Huyo muhuni tu,hana uganga wala bibi yake na uganga,huko Kirando anawaibia watu tu!"
Kamugisha "Kaka sema ukweli!"
Mtanzania "Mi siwatanii,jamaa alikuwa fundi simu,baada ya uongo uongo mwingi nadhani akaona ajifanye mganga ili awaibie watu na kama yuko huko Kirando basi huyo anawaibia sana watanzania!"
Aliendelea "Kama ndiyo huyo anayewafanyia kazi yenu basi mtatapeliwa ndugu zangu huyo dogo hana uganga wowote,Kwanza hapa Kirungu hakuna waganga wengi hapa ni matapeli na wanawatapeli sana watanzania"
Baada ya jamaa kutuambia vile nikakumbuka maneno niliyokuwa nikimwambia Kamugisha kuhusu yule mganga ila kwasababu alikuwa na kichwa kigumu nikabaki nisikilizie.
Kamugisha "Duuuh kaka mbona unanishitua!"
Mtanzania "Labda kawa mganga kweli lakini yule dogo ninavyomjua hana uganga wowote ni mganga njaa tu!"
Aliendelea "We unadhani kwanini hajataka kuwasubiri hapa!,ananijua ndiyo maana kaona asogee huko mbele!"
Kamugisha "Yeye ametuleta kwa mtaalamu mmoja ndiyo tunasubiri tiba"
Mtanzania "Huyo mtaalamu amewaomba hela?"
Kamugisha "Yeah kuna hela tumempa!"
Mtanzania "Aisee mmnahela za kuchezea"
Aliendelea "Ngoja kuna jamaa niwaitie alikuwa fundi mwenzie aje mmulize nisemacho,unajua watanzania huwa wandhani tunawazibia riziki"
Yule jamaa mtanzania alitoka akaelekea mahali ambapo alisema ndipo ilikuwa kibanda cha kutengenezea simu cha Jentre na hakikuwa mbali,jamaa alivyotoka tukawa tunamuangaza Jentre lakini hatukumuona,Kamugisha alichukua simu akampigia akasema ametoka kidogo hayuko mbali na kama tumemaliza tuseme ili aje atupeleke sokoni tukanunue mahitaji,Kamugisha alimwambia asubiri kidogo.
Sasa yule mtanzania haukupita muda akaja ameongozana na mshikaji yuleyule ambaye ndiye tuliamini ni mganga,jamaa baada ya kutuona alitaka kufa kwa presha!
Inaendelea ...................