Namna ya kuandaa saladi

akohi

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Posts
787
Reaction score
526
Mahitaji:

Nyanya
Vitunguu maji
Chumvi
Vinegar
Ndimu
Pilipili mbuzi au kichaa
Parachichi lililoiva lakin liwe gumu
Embe dodo/ lile kubwa lililoiva
Hohoho
Karoti
Kabichi
Tango

Safisha viungo vyote vizuri,

Anza kukatakata vitunguu maji kisha tia ndani ya maji safi ili kupunguza ukari japo wengine huosha na chumvi ila sishauri, viache kwa muda kisha osha na maji safi.

Endelea kukata kata vyote vilivyobaki kisha changanya kwa pamoja then tia vinegar na chumvi then acha kwa muda kuua wadudu, mwisho katakata parachichi

Kisha changanya kwa pamoja.

Embe lazima pia likatwe kwa vipande vidogo vidogo sana.

Hii nzuri kwa wenzangu walevi maana inakata pombe na pia huondoa hang over lakin pia inaongeza hamu ya kula na husaidia tumbo kutojaa gas hata ule vipi au unywe vipi.

Sijaweka vipo maana naamini sote tunauwezo wa kukadiria hahahaha
 

Attachments

  • 1408261628707.jpg
    87.7 KB · Views: 1,573
  • 1408261650019.jpg
    105.3 KB · Views: 1,264
Hahaha, safi sana. Hii hata mdogo wangu wa primary anakupelekeshea bila shida.

Asante mkuu
 
Hehehehe pamoja wakuu, nimejikuta nacheka tu..safi sana Bulldog,

FYI: inabidi niwakaribishe siku moja huku kigamboni tuna umoja wetu wa watu takriban 40 na huwa tunaandaa wenyewe (wanaume) kila kitu from kachumbari mpaka ku foil na kuchoma nyama samaki mishikaki basi ni raha ajabu kukuta akina baba wako busy na visu, same time bia mkononi yaan kata mti panda mti, so lovely guys! Tunafanya kila mwezi
 

Wow!, wonderful!, bora hivi kuliko kukaa tu na kunywa!
 
Mkuu thanks for the best salad, it is really the 'best'
Mara nyingi nakula salad as a meal, so I add peanuts for protein if not meat.
Unaweza pia kutumia lettuce badala ya cabbage cause ni laini zaidi
 
Safi kabisa kui, ila hizi terminology za upishi zinanipa shida, lettuce ndo nini ndugu yangu
 
Safi kabisa kui, ila hizi terminology za upishi zinanipa shida, lettuce ndo nini ndugu yangu

Thanks. It looks yummy.

Lettuce ipo km cabbage kimuonekano lkn ni ndogo. Sana huwekwa kwenye burger
 
Reactions: kui
Safi kabisa kui, ila hizi terminology za upishi zinanipa shida, lettuce ndo nini ndugu yangu

Angel N. Amesema vyema, lettuce ni kama soft version ya cabbag.
 
Yaani nimeangalia hizo picha nikajiuliza huyu ni mwanaume ama? Kachumbari nzuri sana hiyo. Sasa hilo bakuli ndio limenikata stimu. Aisee, ukinipa chakula kitamu kwenye sahani mbaya ya plastic utamu wote unapotea! Hebu muibie mchuchu bakuli banaa, aaaghh
tunaandaa wenyewe (wanaume) kila kitu from kachumbari mpaka ku foil
 

Unamfundisha wizi ati aibe bakuli kwa mchuchu....

Itabidi wachange tu wanunue bakuli la udongo.....
 

ww ndio amada number one
 
Nilifikiri niko peke yangu nikiyekatwa stimu na beseni.
Ila naanza kujiogopa kama nimekuwa picky kama wewe, basi ninapoelekea sio. Lol
 
Duh, nyie kweli bado aisee, hamjui raha ya kujipikirisha hahaha mind u huwa tunafanyia shambani na ni wanaume tu hehehe (nafikiri hapo unaelewa mazingira huwa yanakuwaje?)
 
hahaha farkhina, ukiiba bakuli huachiki bwana weeeeh. Watanunua kwani wanajuaje kama hilo bakuli zuri? Manake hata hichi kibeseni wamenunua lol! nacheka kama mazuri.
akohi, yaani hakuna mwanaume mwenye mvuto kama anaepika (paw anaita preparing food, not cooking). Ila vyombo vizuri makes you exceptional. Nitakununulia zawadi ya bakuli zuri, very stylish la plastic la kuwekea kachumbari manake najua unaogopa kuvunjika. Halafu nitaliacha ofisi za JF. Sawa baba?
Unamfundisha wizi ati aibe bakuli kwa mchuchu....

Itabidi wachange tu wanunue bakuli la udongo.....

Hahahahaaaaa, am i that bad? Sina mpango wa kubadilika. Ila seriously, i have no single plan in changing. Uzuri huwa sitoi opinion yangu, ila nikija kwako ukanipa glass ina mawingu, na ina harufu ya togwa napiga tarumbeta soda.
Nilifikiri niko peke yangu nikiyekatwa stimu na beseni.
Ila naanza kujiogopa kama nimekuwa picky kama wewe, basi ninapoelekea sio. Lol
 
Last edited by a moderator:
Hahaha mi naomba niwaalike mwisho wa mwez huu, nianze na king'ast ili aje na bakuri lenye mvuto hahaha.

Kimsingi huwa vyombo vinabaki shamba ndo maana hatutaki kuingia gharama maana mara nyingi ukirudi hukuti kitu au unapewa story ndeeeeefu na wafanyakazi wa shamba...taabu sana aisee
 
Hahaha mie huko sijiiiii! Labda mumualike paw afu nizamie.

Bakuli ntakununulia 3, ila zikipotea nakuja kufanya timbwili la asha ngedere, waambie kabisaaaa!
 
Hahaha huo mtihani ati, hilo timbwili siwez kulikwepa make uhakika wa kupotea sahani ni 100% hahaha.

Paw. Luksa kuzamia hehehe.
 

Umesema kweli....niliona hilo kabla ya salad ila ilibidi nimezee tu kwa vile ni mkaka.....lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…