Namna ya kuanza Biashara ya kununua na kuuza vitabu

Namna ya kuanza Biashara ya kununua na kuuza vitabu

Joined
Sep 20, 2018
Posts
25
Reaction score
10
Habarini wakuu, nataka nianze Biashara ya kuuza Vitabu vinavyohusu Maisha....inspirational na mahusiano.
Ni sehemu gani naweza pata kwa bei ya jumla? Na Biashara hii ikoje kwa ujumla?
 
mkuu kwanza uko mkoa gani, na pili jaribu kupita sehemu za bookshop uone,na uangalie unawalenga kuwauzia akina nani,soko lako umewalenga akina nani, any way pambana mkuu
 
Kutegemeana na eneo ulilopo unaweza kupata wateja wa aina gani na ni kupitia hiyo tathmi i utajua pa kuanzia.
 
Fanya tafiti za kutosha.

Lakini kwa ujumla wa Tz hatuna utaratibu wa kusoma vitabu vya namna hiyo. Ni wachache.

Labda uchanganye hivyo na vya masomo plus vitabu vya hadithi katika lugha ya kiswahili na Kiingereza ambavyo mtu yoyote ataweza kununua na kusoma.
 
Mkuu kwa wabongo utauza ila jaribu kuwa na kabizness kengine cha kukupa kipato cha ziada maana watz hatupendi kusoma.

Kitabu ki1 mwaka mzima japo sio wote!
 
mkuu kwanza uko mkoa gani, na pili jaribu kupita sehemu za bookshop uone,na uangalie unawalenga kuwauzia akina nani,soko lako umewalenga akina nani, any way pambana mkuu
Niko hapa Dares salaam, ninawalenga vijana hasa walioko vyuoni kwa Shabani niko chuoni pia. Asante kwa ushauri
 
Fanya tafiti za kutosha.

Lakini kwa ujumla wa Tz hatuna utaratibu wa kusoma vitabu vya namna hiyo. Ni wachache.

Labda uchanganye hivyo na vya masomo plus vitabu vya hadithi katika lugha ya kiswahili na Kiingereza ambavyo mtu yoyote ataweza kununua na kusoma.
Asante sana. Nina community ya vijana wanaosoma Vitabu tayari pia nina blog site inayohamasisha usomaji wa Vitabu... Kwa hiyo natarajia kuwa nahamasisha usomaji wa Vitabu na pia kuuza.
 
Tafuta pia waandishi wa vitabu vya riwaya/simulizi, wakuuzie nakala za vitabu vyao kwa makubaliano yatakayowafaa nyinyi nyote wawili.

Unaweza pata mawasiliano ya waandishi kupitia maktaba ya taifa kwasababu kitabu chochote chenye ISBN ya kitanzania lazima utakikuta huko kwa kuwa kila mwandishi anayenunua ISBN kutoka maktaba ya taifa lazima awapelekee maktaba hiyo nakala 3 za kitabu chenye hiyo ISBN ikiwa imechapishwa nyuma ya cover la kitabu husika.

Jitahidi kuuza vitabu vyenye ISBN maana itakusaidia kuwatambua waandishi wa kitanzania waliyoserious na kazi ya uandishi.
 
Biashara hii inaenda sambamba na uhamasishaji wa watanzania kusoma vitabu (mana siunajua hatuna hiyo culture) huku unauza huku unahamasisha kwa kuptia njia mbali mbali kama vile mitandao ya kijamii au uhamasishaji wa physical yaan nyumba kwa nyumba!

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom