SoC04 Namna ya kuboresha elimu Tanzania

SoC04 Namna ya kuboresha elimu Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Otete Joseph

New Member
Joined
May 19, 2024
Posts
3
Reaction score
6
Kumekuwa na mikakati kabambe ya kuboresha elimu nchini Tanzania. Ata hivyo njia hizo bado zinazalisha wahitimu tegemezi kwa serekali katika masuala ya ajira. Hii imepelekea wahitimu wengi kukosa ajira na kuiona elimu kama haina maana. Serikali inaweza kufanya yafuatayo ili kuboresha elimu kwa kipindi kijacho;

1. Kuhamisha mafunzo ya Veta kwenye kambi za Jeshi la Kujenga Taifa.
Serikali iunde sera inayoelekeza mafunzo ya veta kufanyika kwenye kambi za JKT ili mhitimu anapomaliza elimu ya msingi au ya upili akijiunga na JKT arudi na taaluma ya ziada badala ya kurudi na ukakamavu pekee. Hii itasaidia wahitimu wanaokosa sifa pamoja na wenye sifa ya kuendelea na elimu ya juu kupata ujuzi wa awali wa ufundi na taaluma inayoweza kumpa ajira binafsi bila kungoja kuajiriwa. Pia itaokoa Muda na gharama za kwenda VETA baada ya kumaliza mafunzo ya JKT ili kutafuta taaluma ya ufundi.

2. Taasisi za serikali kuanzisha shule za awali na za ufundi.
Tumeshuhudia Jeshi la Wananchi (JWTZ) ikiendesha shule na hospitali. Pia Taasisi za kidini zimekuwa zikifanya hivyo kwa ufanisi mkubwa lakini kwa gharama za juu. Ni vyema sasa taasisi zingine kama Magereza na Polisi nao kutanua wigo kutoka kwenye afya peke yake na badala yake wajenge shule ili wanapoajiri wahitimu wa mafunzo ya JKT na VETA watakaoendelea na Elimu ya juu, wakiwa kazini kazi yao iwe ni pamoja na kusimamia na kufundisha taaluma na ufundi kwa wanafunzi wa elimu ya awali. Hii itapunguza msongamano mkubwa kwenye kambi za JKT na VETA kwa kuwa watakaopitia shule hizo watakuwa tayari wameshapata elimu iyo.

3. Shule binafsi ziwe na masomo ya ufundi.
Kwa Sasa, shule nyingi za watu binafsi hazitoi elimu ya ufundi. Mhitimu anategemea akihitimu ndio atafute chuo akajiendeleze na masomo ya ufundi. Hii inapelekea usumbufu na mlolongo mrefu kwa wahitimu kutuma maombi ya kujiunga na mafunzo hayo. Ikiwa shule binafsi zitaanzisha mafunzo hayo, itarahisisha wahitimu kuweka malengo mapema ya aina ya taaluma ya ufundi anaohitaji kutokana na uwezo wake wa kimasomo alionao shuleni hapo.

3. Masomo ya "art and craft na kilimo" yarejeshwe kuanzia shule za msingi. Umri mdogo ni kipindi ambocho mwanafunzi huelewa zaidi stadi za kazi na mafunzo mengine anayopatiwa. Pia kwa muda huo anakuwa hajawa mbaguzi wa kazi au taaluma fulani. Kuna dhana hujengeka kadri mwanafunzi anavyozidi kukua kwamba wanaochukua masomo fulani wana uwezo mkubwa kiakili kuliko wanaochukua masomo fulani. Hili dhana limepelekea baadhi ya wanafunzi kuchagua masomo wasiyoyamudu ilmradi tu ionekane kwamba amechukua masomo hayo. Ikiwa masomo ya stadi za kazi na kilimo zitaanza kufundishwa kwa vitendo katika elimu ya awali, wanafunzi wenye talanta na mafunzo hayo watafuata mkondo huo mapema kabla ya kuingiwa na dhana ya kubagua masomo fulani na kukimbilia masomo fulani ambazo ata hivyo baada ya kuhitimu hujikuta hazina ajira ya kutosha.

5. Kada ya ualimu iwe na wahitimu wa alama za juu.
Sekta ya elimu imekuwa ikipitia wakati mgumu kuwaajiri wahitimu wengi wanaofaulu masomo yao ya upili kwa alama za juu kwenda vyuoni. Wahitimu wengi wa aina iyo hukimbilia kwenda kusomea"white collar jobs" wakiamini kwamba kazi ya ualimu haina malipo mazuri. Matokeo yake kada hii ya elimu inakimbiliwa na wenye ufaulu wa kati au wa chini na matokeo yake ni kuzalisha wahitimu wenye mrengo hasi wanaoamini kwamba kutofaulu masomo sio mwisho wa maisha bali ni jambo la kawaida.

6. Kupunguza gharama za elimu shule binafsi.
Kama ilivyo kwa mamlaka ya udhibiti wa usafirishaji nchi kavu (LATRA), iundwe mamlaka ya kusimamia sekta ya elimu nchini kwa shule binafsi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba gharama za hizo shule zimekuwa juu mno, wanajipangia ada kwa namna wanavyopenda. Wanapokuwa maeneo yenye upungufu wa shule, wanapanga gharama kubwa zaidi wakijuwa kuwa wazazi watalazimika kuwapeleka watoto wao kwa vile hawana mbadala. Matokeo yake wanafunzi wanaofanikiwa kujiunga nao ni wale wanaotoka kwenye familia zenye uwezo kifedha huku wakiwaacha wasio na uwezo wa kifedha wakisafiri umbali mrefu kwenda kutafuta elimu. Hili hupelekea wanafunzi wengi wa shule binafsi kupata alama nzuri kwenye mitihani ya kuhitimu ukilinganisha na wahitimu wa shule za serikali.

7. Wizara zisimamiwe na wenye taaluma inayoendana na wizara husika.
Kwa sasa wizara nyingi nchini zinasimamiwa na wanasiasa bila kujali taaluma yake. Jambo kama hili hupelekea mwenye taaluma kudharauliwa na mwanasiasa kwa sababu anamzidi cheo na kupelekea wataalamu kuwa watumwa wa kisiasa kazini. Mwisho ufanisi hushuka na hata kufanya wataalamu kuona siasa ni njia rahisi ya mafanikio kuliko taaluma. Ikiwa wizara ya elimu itasimamiwa na watumishi waliohitimu fani ya ualimu, watajuwa matakwa, changamoto na mahitaji ya elimu bora kwa Tanzania kwa miaka ijayo.

8. Bajeti ya elimu iongezwe kukidhi mahitaji yajayo.
Kumekuwa na upungufu wa mahitaji ya elimu kama vitabu na vifaa vingine vya kujifunzia, hii ni nje ya uhaba wa waalimu, madarasa na madawati. Ikiwa bajeti itazingatia mahitaji yote muhimu ya elimu ikiwemo waalimu wa masomo ya hisabati na sayansi, elimu yetu itakuwa bora na kutoa wahitimu walioiva.
 
Upvote 2
1. Kuhamisha mafunzo ya Veta kwenye kambi za Jeshi la Kujenga Taifa.
Serikali iunde sera inayoelekeza mafunzo ya veta kufanyika kwenye kambi za JKT ili mhitimu anapomaliza elimu ya msingi au ya upili akijiunga na JKT arudi na taaluma ya ziada badala ya kurudi na ukakamavu pekee
Hio ni jema sana. Majeshi yawe ni kulijenga taifa kila idara.

Ni vyema sasa taasisi zingine kama Magereza na Polisi nao kutanua wigo kutoka kwenye afya peke yake na badala yake wajenge shule ili wanapoajiri wahitimu wa mafunzo ya JKT na VETA watakaoendelea na Elimu ya juu, wakiwa kazini kazi yao iwe ni pamoja na kusimamia na kufundisha taaluma na ufundi kwa wanafunzi wa elimu ya awali
Matumizi mazuri ya akili na nguvu ndio haya sasa.

Kada ya ualimu iwe na wahitimu wa alama za juu.
Sekta ya elimu imekuwa ikipitia wakati mgumu kuwaajiri wahitimu wengi wanaofaulu masomo yao ya upili kwa alama za juu kwenda vyuoni. Wahitimu wengi wa aina iyo hukimbilia kwenda kusomea"white collar jobs" wakiamini kwamba kazi ya ualimu haina malipo mazuri.
Na ni kweli. Anayefundisha anatakiwa awe nondo kwelikweli. Ila vifurushi viwe vya kuwavutia sasa huko.

Wizara zisimamiwe na wenye taaluma inayoendana na wizara husika.
Kwa sasa wizara nyingi nchini zinasimamiwa na wanasiasa bila kujali taaluma yake
 
Walimu walipwe vizuri,ili fani ya elimu isudharaulike. Hii ita attract watu competent

Mkuu hilo la shule binafsi libaki hivyo hivyo ada Iwe juu..wanaingia costs kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia, kuwalipa walimu wazuri etc ...serikali ikiweka miundo mbinu bora kwa shule zake ndio itaregulate kiasi cha ada wanachotoza shule binafsi, since kutakuwa na ushindani kupata wanafunzi, na sio kuwalazimisha wapunguze ada sasa hivi. Pia ni jukumu la serikali kujenga shule sehemu zote. Binafsi nimeona hapo umejaribu kuwatupia mzigo shule binafsi wakati serikali ndio iko responsible. Otherwise ni bandiko Zuri nimekupa vote.
 
Back
Top Bottom