SoC04 Namna ya kuhifadhi mazao mepesi kuharibika (perishable crops) baada ya kuvuna

SoC04 Namna ya kuhifadhi mazao mepesi kuharibika (perishable crops) baada ya kuvuna

Tanzania Tuitakayo competition threads

Amos robert

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
3
Reaction score
2
Utangulizi; mazao mepesi kuharibika ni nguzo imara ya kipato kwa wafanya biashara wadogo wadogo kama vile mbogamboga na matunda, lakini changamoto kubwa ni kuharibika kwa uharaka hasa yawapo sokoni jambo ambalo hupelekea hasara kwa wafanya biashara hawa.

Utatuzi; ili tuweze kuishi Tanzanian tuitakayo, njia pekee ya kukomboa na kuepusha kuharibu kwa hayo mazao ni juu ya ubunifu wa kutumia kimiminika cha mkaa katika kuhifadhi mazao hayo badala ya kutumia majokofu ambayo wafanya biashara wa aina hii hawana uwezo wa kununua hayo majokofu kwaajili ya kunusuru mazao yao yawapo sokoni, lakini kwa kututumia kimiminika hiki mtu yeyote anaweza kuwanacho aidha shambani,sokoni na hata majumbani na kufanya mazao haya yaweze kukaa muda mrefu bila kuharibika. Hivyo serekali ikiweza kuhimiza juu ya matumizi ya hiki kimiminika mkaa wafanya biashara wa mazao haya watakuwa na uhuru wa kuweka mzigo wa mkubwa sokoni bila kuwa na hofu ya kuharibika endapo soko litayumba,


Faida ya kimiminika mkaa katika kuhifadhi mazao mepesi kuharibika ni pamoja na
1. kuyaweka mazao katika hali yake harisi kama yawapo kwenye shina kwa muda mrefu
2. Kutoa sumu zote hasa za madawa yaliyo tumika kukuzia mazao hayo wakatiki yakiwa shambani

Mazao haya kwasasa hutumia kemikali mbalimbali toka kupandwa,kukuzwa mpaka kuvunwa kwake,na ukizingatia ni mazao ambayo hupendwa kuliwa yakiwa mabichi( mfano nyanya,karoti ambavyo hutumika katika kachumbari, mboga za majani ambazo huwa hazichemshwi sana)

Hitimisho
Matumizi sahihi ya kimiminika hiki kitaokoa namba kubwa ya wanawake hasa wanaojihusisha na biashara ya mbogamboga hapa nchni hivyo kuinua uchumi kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa kwa ujumla
 
Upvote 2
njia pekee ya kukomboa na kuepusha kuharibu kwa hayo mazao ni juu ya ubunifu wa kutumia kimiminika cha mkaa katika kuhifadhi mazao hayo badala ya kutumia majokofu
Ninaona dalili ya kufundishwa kitu kipya hapa. Ngoja nichimbe..... shusha nondo broh💪🏿.

Matumizi sahihi ya kimiminika hiki kitaokoa namba kubwa ya wanawake hasa wanaojihusisha na biashara ya mbogamboga hapa nchni hivyo kuinua uchumi kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa kwa ujumla
Heeeeh!!! We jamaa, unahitimoshaje na haujatuambia hiyo teknolojia ipoje. Rudi haraka sana ujazie nyama watu tuelewe.
 
Back
Top Bottom