Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Hapa nazungumzia kuimarisha mapenzi katika mahusiano ya kawaida au kwa namna nyingine mahusiano ambayo sio ya kimapenzi
Kwanza ni kuonyesha unavutiwa na mambo ya rafiki zako au watu ambao huwa mnakuwa pamoja,nikwambie kitu expert?
Hakuna watu ambao hawapendi kujua kwamba upo interested na mambo yao,mfano kuulizia familia zao zinaendeleaje,kama ni mtu ambaye alikwambia kuhusu jambo lake fulani basi ukamuuliza vipi biashara inaendeleaje au ufugaji unaendeleaje
Kwa kufanya hivyo unaonyesha unajali na kuwafanya wavutiwe na wewe na wakupende,kwahiyo onyesha kujali nao watakupenda pia
Jambo la pili,ni kuwa na uso wa bashasha mara ukutanapo na wapendwa wako,onyesha uso mkunjufu na kuonyesha umefurahi kuwaona,ongea nao kwa tabasamu,hakika watajisikia vizuri na kufurahi kampani yako,na utaimarisha mahusiano yenu
Jambo la tatu ni kujichanganya na watu,usiwe mtu wa peke yako peke yako tu,sometime unajichanganya na watu na kujenga urafiki na mazungumzo ya hapa na pale,ebu angalia watu ambao ni wacheshi na waongeaji huwa wanazoeleka mapema na kupendwa na watu
Ni hayo tu!