Namna ya Kukomesha Rushwa Tanzania

Mkuu, siamini kuwa kwa kuwa na adhabu kali kama China kutasaidia kupunguza au kufuta matendo ya rushwa nchini.

China ambao wanayo adhabu ya kifo kwa rushwa kubwa, wameweza hata kumhukumu Waziri wao Mkuu kwa vtendo hivyo vya rushwa. Lakini nao pia, hawawezi kusema kuwa hawana rushwa katika system zao. Rushwa ipo China.

Kinachotokiwa kufanya, ni kuhakikisha kuwa mianya ya rushwa inadhibitiwa. Utaratibu mzuri wa manunuzi ya umma (utaratibu ambao ni lazima uheshimiwe na kila mtendaji wa serikali na mashirika ya umma).

Kuwe na usimamizi usio na woga, wala upendeleo wa matumizi na mipango ya matumizi/manunuzi ya umma. PPRA ipewe nguvu za kisheria na isimamiwe katika kuzitekeleza nguvu zake, ili kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali za Taifa.
 
Recta, Tatu na Wengine,

Nawashukuru kwa michango yenu. Natumaini wahusika watafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa kuanzia kuwa na adhabu kali, kufilisiwa kwa wala rushwa, mikataba yote kuridhiwa na BUNGE, PPRA kupewa nguvu zaidi za kisheria na uwezo na kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa kama inavyopasa. Wabunge tunaomba mtusaidie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…