Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 42
Mkuu, siamini kuwa kwa kuwa na adhabu kali kama China kutasaidia kupunguza au kufuta matendo ya rushwa nchini.SHUPAZA,
Uzuri ni kwamba wenzetu hawana mchezo katika suala la rushwa. Mfano mzuri ni China. Tanzania tunaweza. Ni wakati sasa wa kuamua na kutenda.
Itakapobidi kama mambo hayabadiliki tunaweza hata kufikiria kuwa na ADHABU YA KIFO KWA MAKOSA YA RUSHWA. Kama adhabu ya ATTEMPTED RAPE ni kIfungo cha Maisha kwa nini kosa la Rushwa ADHABU YAKE ISIWE KIFUNGO CHA MAISHA NA VIBOKO VYA KUTOSHA AU HATA KIFO?
Tuanzishe adhabu hii tuone kama hali haitatengemaa. Ikiwezekana tuwe na MAHAKAMA MAALUM KWA AJILI YA MAKOSA YA RUSHWA NA UFUJAJI WA RASILIMALI ZA NCHI PAMOJA NA UTUMIAJI MBAYA WA MADARAKA.
China ambao wanayo adhabu ya kifo kwa rushwa kubwa, wameweza hata kumhukumu Waziri wao Mkuu kwa vtendo hivyo vya rushwa. Lakini nao pia, hawawezi kusema kuwa hawana rushwa katika system zao. Rushwa ipo China.
Kinachotokiwa kufanya, ni kuhakikisha kuwa mianya ya rushwa inadhibitiwa. Utaratibu mzuri wa manunuzi ya umma (utaratibu ambao ni lazima uheshimiwe na kila mtendaji wa serikali na mashirika ya umma).
Kuwe na usimamizi usio na woga, wala upendeleo wa matumizi na mipango ya matumizi/manunuzi ya umma. PPRA ipewe nguvu za kisheria na isimamiwe katika kuzitekeleza nguvu zake, ili kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali za Taifa.