SoC01 Namna ya kukuza uchumi(inclusively), kuleta ajira na fanaka kwa Watanzania

SoC01 Namna ya kukuza uchumi(inclusively), kuleta ajira na fanaka kwa Watanzania

Stories of Change - 2021 Competition

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Kwa muda mrefu watu tumekuwa tukizungumza namna mbalimbali za kukuza uchumi kuongeza ajira ili kila mmoja afaidike kwenye keki ya taifa. Nimeona si haba na mimi nikitoa mawazo yangu katika namna ambayo watu wengi watapata ajira.

DHANA YA MAENDELEO
Maendeleo ni uwezo wa mtu kuamrisha vitu, hii ni maana aliyoitoa mchumi nguli wa maendeleo Amartya Sen ambayo nakubaliana nayo, kwa maana ya kwamba, uwe na uwezo wa kuamrisha maji yaje nyumbani kwako, sio maji yakuamrishe wewe uende kisimani. Uwe na uwezo wa kuamrisha chakula chako, sio chakula kikuamrishe nk nk.

Wakati huo watanzania vitu vingi tumeshindwa kuviamrisha, lakini naona iko fursa kwa baadhi ya vitu kuweza kuviamrisha ili kufungua uchumi. Mfano wa jambo la kuanza nalo ni ujambazi, Polisi wetu nchini mbali na kufanya kazi nzuri wameshindwa kuamrisha ujambazi badala yake majambazi wanatuamrisha sisi, mfano mzuri ni kuwa gari za abiria zilizuia kutembea usiku kwa sababu tu ya ujambazi, yaani tumekubali majambazi watupangia muda wa kufanya shughuli za kiuchumi badala ya sisi kuwadhibiti ili uchumi uendelee, na kwa kuwa tumetii amri ya majambazi ni kweli shughuli nyingi zinafungwa mida fulani.

KUFUNGUA UCHUMI
Moja kati ya jambo zuri la kufungua uchumi ni kuruhusu shughuli zifanyike masaa 24, siku saba za wiki. Jamani ni wazi kuwa, ukifinya muda wa kazi umefinya uchumi, mmeona lockdowns na curfews zilivyoathiri uchumi wa nchi kadhaa. Hivyo ufunguzi uanze kwa kufanya kila mtu afanye shughuli saa 24 bila kuzuiwa na sheria badala yake ni yeye mwenyewe aone kuwa anapaswa kufunga kwa sababu zake

Hapa panahitaji polisi watusaidie kwa kiasi kikubwa kwa kufanya proper allocation ya nguvu zao, yani badala ya kuanza kutafuta ‘wazurulaji’ waanze kuhakikisha majambazi hawabugudhi watu kwenye kila eneo. Mathalani kwenye mambo ya mabasi yatakayokuwa yanatembea usiku, askari watapaswa kupiga doria barabara korofi ili kuhakikisha usalama wa wasafiri.

Shughuli za klabu na bar nk, ziende saa 24, mtu asipangiwe muda wa kunywa kwa kuwa tunakazi tofauti tofauti kuzuia pombe kufanywe na kampuni au ofisi, yaani waseme wao kuwa hakuna mtu kwenda kazini akiwa amelewa

Kama mnakumbuka redio zilikuwa zinfanya kazi mwisho saa sita usiku, lakini kwa sasa ni saa 24 na mnaweza kuona namna ajira redio zilivyoongeza watu katika ajira.

MATOKEO TARAJIWA
Ieleweke kuna watu wanakazi usiku lakini huwa wanashindwa kutoka kwa kusema usafiri usiku unasumbua, au chakula usiku hakipatikani hii ni kwa kuwa wateja na wauzaji wanahiyo ali ya kuona kazi mwisho muda fulani, labda kwa siku hizi watu wa bodaboda baadhi ya maeneo ndio hufanyakazi saa 24, na watu kadhaa kwenye stendi za mabasi wamekuwa wakitoa huduma saa 24. Suala la huduma hizi zisibaki Stendi za Mabasi pekee bali kila sehemu watu wawe na uhakika wa usalama na kufanya mada zao.

Hivyo basi watu watapata ajira kwa kuwa kutakuwa na utanuzi wa biashara na shughuli zilizoko na watakaokuwa wanatembea usiku wataongezeka na kufanya shughuli ziongezeke zaidi na zaidi.

AMANI ITAFSIRI MAENDELEO
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiamini kuwa Tanzania kuna amani hadi hivi karibuni ambapo niliulizwa kuwa nazungumzia amani gani na rafiki yangu ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi akishuhudia amani kubwa huku nchi hizo zikiwa hazijisifu kuwa tuna amani au la.

Swali niliulizwa, kama sisi tuna amani, je unaweza kutembea na baiskeli kwenda kokote unakotaka saa nane usiku? Jibu ambalo kila mtu analijua wakati huko kwa wenye amani ni kawaida kuwaona watu, mabinti(inclusive) wakitembea na baiskeli usiku bila hofu, wakati huo kwetu utakamatwa uzururaji na askari wa doria wa usiku. Amani itafsiri maendeleo.

MAENDELEO NI UHURU
Kama nilivyofungua ndivyo ninavyofungwa kwa kumtumia Amartya Sen kuwa maendeleo ni uhuru, uhuru wa kuwa na maamuzi, uhuru wa kuamua, uhuru wa kutembea nk nk. Ndio sababu iliwekwa kwenye uwezo wa kuamrisha, kwa kuwa uwezo wa kuamrisha unatafsiri uhuru kutoka kwenye Micro-Level hadI Macro-Level. Sheria nyingi ambazo zinazuia uhuru wa mtu bila kuwa na matokeo katika uchumi ni sheria za ajabu.

Ieleweke kuwa sekta zisizo rasmi zimeajiri watu wengi kuliko sekta rasmi(Angalieni data NBS) kwa mantiki hiyo huwezi mkamata mtu ambaye anatembea usiku na kusema mzururaji kwa kuwa hana kitambulisho wakati inawezekana yuko sekta isiyo rasmi aidha vitambulisho viko kwa watu wachache mtu akamatwe kwa kosa lenye maana sio kwa kutembea usiku.

Niwashukuru wote. Niwaombe msome vitabu vifuatavyo kuhusu Uchumi wa Maendeleo(Development Economics) nilivyoanisha hapa chini.

Akhsanteni

Bibliography​

Todaro, M., & Smith, S. C. (2020). Economic Development. Boston: Pearson Education Limited.
Sen, A. (2014). Development as freedom (1999). The Globalization and Development Reader: Perspectives on Development and Global Change, 525.


Signed

OEDIPUS
 
Upvote 0
Back
Top Bottom