Namna ya kuondosha sumu ilio katika muhogo

Namna ya kuondosha sumu ilio katika muhogo

tilmikha

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2013
Posts
496
Reaction score
604
Muhogo ni chanzo cha tatu cha chakula baada ya mchele na mahindi barani Africa . Na sasa chakula hichi kimejipatia umaarufu mkubwa mno baada ya kuhusishwa na faida kabambe kwa jinsi ya kiume. Lakini wengi sijui kama tunajua kuwa muhogo una sumu aina ya cyanide ambayo inaweza kusababisha hata kifo.

Mpendwa msomaji, huu muhogo mbichi unaopigiwa chapuo katika mtandao ya kijamii ndio wenye kiwango cha juu zaidi ya sumu kuliko uliopikwa. Unaweza ukastajabu kuwa hujawahi kusikia ripoti ya kifo au madhara yaliosababishwa na sumu itokanayo na chakula hichi adhimu lakini hilo haliondoi ukweli kuwa muhogo unasumu. Wazee wetu walikua wanaundaa muhogo kupitia hatua zifuatazo mpaka kufikia hatua ya kuliwa.

Unamenywa hapo tayari kiwango cha sumu ilo katika maganda imetolewa, halafu unarowekwa, Kisha unachemshwa halafu maji yake kutolewa na hapo unaweza kuongezewa nazi ama kuliwa bila ya nazi. Ila unapokula mbichi jua umechukua kiwango kikubwa cha sumu. Na kadiri utakavyokua mchungu ndio kadiri ya kiwango kikubwa cha sumu.
 
Swadakta mkuu wewe hujawahi sikia watu walokufa kwa mihogo ila wengine tumejionea na kusikia kwa watu wa nyanda za juu kaskazini ni mashuhuda wa hilo, mihogo kwa upande wa Kilimanjaro ni miongoni mwa vyakula ambavyo baadhi ya watu hawathubutu kugusa kabisa,
Na ambao wanakula lazima ilowekwe na ikaushwa ndo inatumika kwa chakula kama kusagwa na kuchanganywa na mahindi ama ndizi na kufanywa unga kwaajili ya ugali. na kunabaadhi ambao hula huo ugali na kulewa kabisaa. Hiyo kitu inaogopwa kabisa kunafamilia iliwahi poteza watoto 3 kisa mihogo ya kuchemsha na hata maganda ya mihogo hapewi mnyama kama hapa dar unaona mbuzi na ng'ombe anarushiwa na hadhuriki
.
 
Inategemea na aina ya mihogo yenyewe inabanduliwa maganda yake inalowekwa kidogo then kwenye sufuria, lakini mimi napenda mhogo ukaushwe then ukasagwe unga upikwe uchanganywe na unga wa mahindi hutaona hata hiyo sumu.
 
Hatari mimi niliwashuhudia hao waliolewa ila kifo ndio nakusikia wewe japo najua hio sumu inaua

Back
Top Bottom