tilmikha
JF-Expert Member
- Feb 27, 2013
- 496
- 604
Muhogo ni chanzo cha tatu cha chakula baada ya mchele na mahindi barani Africa . Na sasa chakula hichi kimejipatia umaarufu mkubwa mno baada ya kuhusishwa na faida kabambe kwa jinsi ya kiume. Lakini wengi sijui kama tunajua kuwa muhogo una sumu aina ya cyanide ambayo inaweza kusababisha hata kifo.
Mpendwa msomaji, huu muhogo mbichi unaopigiwa chapuo katika mtandao ya kijamii ndio wenye kiwango cha juu zaidi ya sumu kuliko uliopikwa. Unaweza ukastajabu kuwa hujawahi kusikia ripoti ya kifo au madhara yaliosababishwa na sumu itokanayo na chakula hichi adhimu lakini hilo haliondoi ukweli kuwa muhogo unasumu. Wazee wetu walikua wanaundaa muhogo kupitia hatua zifuatazo mpaka kufikia hatua ya kuliwa.
Unamenywa hapo tayari kiwango cha sumu ilo katika maganda imetolewa, halafu unarowekwa, Kisha unachemshwa halafu maji yake kutolewa na hapo unaweza kuongezewa nazi ama kuliwa bila ya nazi. Ila unapokula mbichi jua umechukua kiwango kikubwa cha sumu. Na kadiri utakavyokua mchungu ndio kadiri ya kiwango kikubwa cha sumu.