Namna ya kupata vibarua na ajira za muda mfupi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Tunaishi kwenye dunia ya utandawazi. Mara nyingi nyumbani hatuna kazi nyingi kila siku. Tulilazimika kuajiri wasaidizi na kuishi nao kwasababu za kiulinzi na usalama.

Sikuhizi apartments nyingi zina uhakika wa ulinzi na usalama na hivi vyote vinakuwa sehemu ya kodi. Zile kazi za kufua kama huna mashine na kupiga pasi, kuosha gari nk

Wakati huo huo kuna vijana hawana hata pesa ya kula. Wanatafuta kazi kama kupanda maua, kupanda mchicha ma mboga mboga, kufua, kupiga pasi, kuosha gari.

Ninafikiria namna ya kuweka mtandao wa kutafuta kibarua wa kumlipa kwa siku.

Changamoto hapa ni uaminifu. Umpate kibarua aondoke na Shula za Louis Vuitton unaweza kupata heart attack.

Ninategemea mawazo yenu jinsi ya kufanikisha wazo hili.
 
Nina Concept Note niliandika na namna watakavyokua recruited, trained, retained and vetted. Nika-share na Wapuuzi flani wakaingia nayo mitini.
Hapa ni lazima ujue jinsi ya kujitangaza na kuwapata wateja. Vibarua wakikosa kazi muda mrefu wanatafuta maisha mengine.

Pia kuwalinda na vitendo vya ubakaji. Kuna wateja wakware.
 
Tengeneza app kama ya uber,anayehitaji kufanyiwa kazi anapiga simu ofisini kwako....wewe ushakusanya vijana waaminifu unawapangia sehemu za kwenda kufanya kazi.

Vijana wanatakiwa wawe waaminifu walete barua ya uthibitisho wa makazi,wadhamini n.k,ili ikitokea kapitiwa na ibilisi akadokoa mali ya hao mafisadi anatafutwa kirahisi.
 
Nje ya mada. Vijana mjini kulala njaa kupenda. Mathalani kwa dar, Kuna wale jamaa wanaonyesha parking za kupaki magari k/Koo, asee wanapiga si haba. Akikuonyesha parking unampa hero/buku halafu wewe utamalizana na mtoza ushuru. Kwasku hawakosi kuanzia ten.
 
Kuweka mfumo wa kupata vibarua na kuwalipa kwa siku au short term contact.
Sawaa mkuu..

Naamini kila kitu kinawezekana kikubwa ni ideas tu.

Hyo project ikikamilika naomba niwe miongoni mwa utakao waajir Kama kibarua Nina sifa ya uaminifu.
 
Ni wazo zuri sana lakini vibaka unawachuja vipi ili wateja husika wasilizwe?

Tunaishi kwenye dunia ya utandawazi. Mara nyingi nyumbani hatuna kazi nyingi kila siku. Tulilazimika kuajiri wasaidizi na kuishi nao kwasababu za kiulinzi na usalama.

Sikuhizi apartments nyingi zina uhakika wa ulinzi na usalama na hivi vyote vinakuwa sehemu ya kodi. Zile kazi za kufua kama huna mashine na kupiga pasi, kuosha gari nk

Wakati huo huo kuna vijana hawana hata pesa ya kula. Wanatafuta kazi kama kupanda maua, kupanda mchicha ma mboga mboga, kufua, kupiga pasi, kuosha gari.

Ninafikiria namna ya kuweka mtandao wa kutafuta kibarua wa kumlipa kwa siku.

Changamoto hapa ni uaminifu. Umpate kibarua aondoke na Shula za Louis Vuitton unaweza kupata heart attack.

Ninategemea mawazo yenu jinsi ya kufanikisha wazo hili.
 
Mfumo kama huu niliuona Kenya unatumika na umefanikiwa vizuri sana.
Na kuna wamama watu wazima kabisa nilikuwa nawaona kwenye mageti ya mabosi wakisubiria hiyo ya day work(temporary house maid) na wanalisha familia zao na kusomesha watoto.
Kilichowafanya wafanikiwe ni kwa sababu wakenya wana discpline sana ya kazi na kila mtu anaheshimu kazi ya mwingine.
Tatizo linalokuja bongo sasa ni ukosefu wa discpline kwenye kazi na baadhi ya watu kudharau au kuchukulia powa/masihara kazi ya mwingine.
Sitaki nikuvunje moyo unaweza kuifanya ukaangalia trend yake but I guess utakuwa unaletewa kesi za ajabu sana ambazo zingine utashindwa kuzipatia ufumbuzi.
Na kesi ambazo utazipata mara kwa mara ni
1.Wizi-wabongo huwa hawaheshimu future yao yaani yuko tayari kuacha kazi inayomuingizia kipato miaka yote kwa kuiba na kutoroka kwa kitu chenye thamani ya laki 5.
2.Kupeana mimba-wenye majumba huwa hawana nidhamu ya kuheshimu umuhimu wa kazi ya housemaid huwachukulia kama watumwa na kuwafanya watakavyo.
3.Kukosekana au kuchelewa kwa malipo-wenye nyumba wengi walishazoea kulipa elfu 30 au 40 kwa mwezi mzima na tena sio kwa wakati hadi muda wanaojisikia,kwa hyo wewe ukiwaambia wakulipe elfu 10 kwa siku au elfu 50 kwa wiki ili ufidie gharama za ofisi wataona ni mzigo mzito upande wao.
OTHERWISE NI IDEA NZURI

Back
Top Bottom