Dr PL
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 327
- 537
Unene uliopitiliza unaongezeka kwa kasi sana miongoni mwa watu wengi kwa sasa. Hali hii huwaweka watu ktk hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa mfano magonjwa ya moyo, mfumo wa upumuaji pamoja kuathiri uwezo wa mtu kufanya shughuli zake za kila siku.
Kinachosababisha/kuchangia unene ni mtindo wa maisha hasa ulaji, yaani aina ya vyakula ambavyo watu hutumia ukilinganisha na shughuli zao za kila siku. Mwili unapokea kitu chochote kwa zaidi ya kiwango kile kinachotakiwa basi kile cha ziada huhifadhiwa mwilini kama mafuta ambayo ndio unene.
Ulaji wa vyakula vya wanga (ugali, wali, mikate, chips nk) kwa watu ambao shughuli zao za kila siku ni za kukaa tu ukilinganisha na wale wanaofanya kazi ngumu kama vile kubeba mizigo, wakulima shambani nk huchangia sana watu hao kuwa na unene uliopitiliza.
Ili kuzuia au kuondoa unene uliopitiliza ni lazima kuzingatia haya.
Kula mlo kulingana na shughuli zako: epuka au punguza wanga hasa kwa wale ambao shughuli zao ni za kukaa ofisini (sedentary lifestyle), vyakula kama matunda na mbogamboga na wanga kidogo uzingatiwe.
Punguza mlo unaopata kwa siku: kama unakula mara 3 au zaidi kwa siku basi unaweza ukapunguza ukawa na milo miwili kwa siku. Hii itasaidia mwili kutumia ile wanga ya ziada hivyo kupunguza unene.
Jali muda wa kula: muda wa kula na aina ya chakula unachokula ni muhimu sana kuzingatiwa. Mfano inashauriwa kuepuka kula vyakula vya wanga usiku, hii ni kwa sababu wakati wa usiku ukilala mwili unakuwa mapumzikoni kwa hiyo matumizi ya wanga yanakuwa kwa kiwango kidogo sana. Ni muhimu ukala matunda usiku au hata ukalaa bila kula (kama utaweza).
Fanya mazoezi: mazoezi ni muhimu sana ktk kuhakikisha kwamba kile kinachoingia mwilini kinatumika ipasavyo. Mazoezi pia hupunguza unene uliopitiliza na kusaidia kuondoa sumu mwilini, lakini usitarajie matokeo ya haraka sana bali matokeo huja taratibu. Watu wengi huweka lengo la kufanya mazoezi na kutegemea matokeo chanya ndani ya muda mfupi sana hivyo wasipoona hukata tamaa na kuacha kuendelea na mazoezi. Jenga utamaduni wa kufanya mazoezi kila siku (mazoezi kama kukimbia, kuruka kwamba, kutembea nk), weka ratiba na zingatia kisawasawa.
Pia kuna njia za kisasa za kupunguza au kuondoa unene mfano kuwekewa puto au kufanyiwa upasuaji.
Muhimu sana: kama unafanya mazoezi au kuzingatia lishe basi hakikisha unaonana na wataalamu (madaktari, wataalamu wa lishe na mazoezi) ili wakushauri namna nzuri ya kufanya kila mchakato wa kupunguza unene uliopitiliza.
Njia zote za kupunguza unene uliopitiliza huhitaji kuendelezwa na kuzingatiwa sana kwa ajili ya matokeo chanya. Ni muhimu kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ktk familia kwa sababu kama watoto watakuzwa kufanya mazoezi (mfano kutembea walau kila siku nk) watapenda kufanya hivyo baadae wakiwa wakubwa hivyo kuwaepusha na unene uliopitiliza.