Ni wazi kuwa migongano katika ndoa hutokea , lakini tatizo huwa ni namna ya kusuruhisha migongano hiyo. Katika ndoa mnaweza kukwaruzana kitu kidogo sana lakini kisipotafutiwa utatuzi mapema kinaweza leta madhara na kuvuruga uhusiano. Kama wewe ni mwanandoa na imetokea umemkwaza mwenzio kiasi cha kumfanya akasirike unaweza kujaribu hii. Mkiwa kitandani huku umemsogelea kwa sauti ya upole mwombe msamaha huku ukionyesha kweli unajutia kile ulichofanya. Mwambie maneno matamu yatakayompa faraja. Usiishie hapo mwonyeshe hisia zako za kimapenzi kwake. Muhimu zaidi mpe mapenzi motomoto siku hiyo. Ukitoka hapo hakuna atakayetaka kuanza kujadili kuhusu kosa hilo. Huu ni mtazamo wangu na imenisaidia binafsi. Matatizo mengine yanaweza kumalizwa na wanandoa wenyewe sio lazima kuwashirikisha watu wengine.