Namna ya kusitisha matumizi ya TIN namba TRA

Namna ya kusitisha matumizi ya TIN namba TRA

Andika barua ya kulifunga duka lako sababu ni kufilisika.w
 
nenda kwa serikali yako ya mtaa wajulishe una fynga biashara mambo yamekuwa magumu, mtendaji baada ya kuthibitisha umefunga biashara yako atakuandikia barua ya kupeleka TRA, nawe utaandika barua nakala kwa afisa biashara wilaya kwenda ofisi ya TRA ambako biashara tin yako imesajiliwa,

hapo tin yako itasitishwa, na hali itakaporejea kuwa vyema utaweza endelea na tin hiyo hiyo bila kuwa na deni tra na kwa leseni
Mbona niliwahi kwenda Ofisi moja ya TRA kuwaeleza nataka kufunga Biashara wakanieleza kuwa niende kwa Mkurugenzi husika aliyetoa leseni ya Biashara ndiyo anipatie barua juu ya kufunga/kusitisha biashara ili wao waweze kufanyia kazi.Aidha, unatakiwa kuwasilisha Certificate origional (TIN-TRA) na LESENI (Mkurugenzi) pia.
 
Leseni ya Biashara inahusiana nini na wao? kama leseni ako ime expire mtoa leseni hakutambui asilani
 
Wanajf mimi pamoja na kuwa muumini mzuri wa kulipa kodi hali inazidi kuwa mbaya.Mwezi julai wakati naanza kuuza haka kagenge nilikuwa nauza hadi sh.80000/= kwa siku nikaenda TRA wakanipa tin namba.Manisipaa wakanipa leseni nikawa full hapa kazi tu!!!!Ajabu kuanzia oktoba mosi mauzo yameshuka hadi sh.7000/= kwa siku.Wadau nisaidieni namna ya kufanya ili niisitishe hii tin namba kwani sitaweza kupata kodi waliyoniambia ya sh.318000/=ifikapo Desemba 2016
biashara ya genge nayo unalipa TRA!!! Au ulikodi frem ndg? Ukitaka usilipe kodi,tafuta eneo zuri jenga genge lako la miti hapo hawatakusumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapa ndiyo JF, ukiomba ushauri usishangae kukutana na watu wanaojifanya wanajua kila kitu na kauli za kukubeza.
Nakushauri kitu kimoja, funga hiyo biashara (japo kwa muda), then andika barua kwa meneja wa TRA mkoa uliopo ukimtaarifu kwamba UMEFUNGA biashara kwa sababu biashara haiendi vizuri hivyo umeishiwa mtaji na kufikia maamuzi ya kuifunga biashara hiyo kwa sababu imefikia kipindi unaiendesha kwa hasara, onesha dhahiri ni kuanzia tarehe ngapi umesitisha rasmi kufanya biashara. Inategemeana na ulipo na aina na ukubwa wa biashara uliyokuwa unafanya, huenda wakafika kukagua kujiridhisha kama kweli umefunga. Baadaye ukibuni biashara nyingine unaweza kujisajili upya na wakakufanyia makadirio upya (wengi wanatumia ujanja wa kutumia jina tofauti kabisaa, hata maafisa wa TRA wanalijua hilo). Kama biashara kweli hailipi kabisa achana nayo mkuu, fanya biashara nyingine.
Sasa akifunga hiyo biashara,si ataikosa hata hiyo 7000 anayopata kwa siku? Kwa mauzo haya ya siku,nadhani hatotakiwa kulipa kodi kabisa kwa maana hesabu za mwaka hazizidi million 4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa akifunga hiyo biashara,si ataikosa hata hiyo 7000 anayopata kwa siku? Kwa mauzo haya ya siku,nadhani hatotakiwa kulipa kodi kabisa kwa maana hesabu za mwaka hazizidi million 4

Sent using Jamii Forums mobile app
Kodi atalipa tu, kama anaweza kulipa pango la duka na tra wanataka chao!
 
[emoji4] [emoji4] [emoji4] mi nimemshauri ahame frem,ajenge banda la miti kama magenge mengine TRA hawatomsumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahhaa. Lakini yeye aliuliza namna ya kusitisha TIN number yake, labda ili akija kutaka kufanya biashara tena asijekutana na deni kubwa, maana usipoandika barua ya kufunga biashara TRA wanaendelea kuhesabu deni na fine kila mwaka!!
 
Yah,afatilie namna ya kusitisha hiyo TIN akishafanikiwa ahame hapo aendelee na biashara yake bila kusumbuana tena na tra

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida yang naomba msaada jamanin simesahau tin number yangu na laini Yang imepotea
 
Back
Top Bottom