Shambaboy jogoli
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 1,223
- 1,627
Ach
Tulieni dawa iwaingie, si mnajifanya wajanja, ukisimama mshale ukikimbia mshale! Nyie na mabeberu wenu acha korona feki iwapige na humu sie tunawapiga humu tukichapa kazi!Kenya iliposema lazima kila Mtanzania anayekuja huku apimwe kwanza, Watz walipiga makelele sana humu, wakafunga mipaka,
wakalipuka lipuka kwa kauli za kiajabu, ila baadaye walikubali yaishe maana hadi leo hakuna anayepita huo mpaka bila kupimwa, labda wanaotoa hongo kwa polisi wetu mafisadi.
Kwa ndege pia itumike hiyo njia, kila anayeng'ang'ania kuja, akubali kupimwa, maana kwao huko walishajichokea kwenye hili la corona na kuachia kila kitu, wa kufa ajifie na wa kupona apone, sasa ili kuzuia wao kutuletea balaa lao hilo, tukomae kama tulivyofanya kwa mpakani, kwa sasa watafanya mengi ikiwemo kuzuia ndege zetu lakini tusisahau sababu za sisi kuwazuia kuja huku, sio kwamba tuna chuki nao, ila afya yetu ni kipau mbele.
Serkali iingie kwenye mazungumzo na uongozi wao kimya kimya na kufikia hayo maamuzi ya kuhakikisha kila mmoja wao anapimwa.