Mkuu hivi wakisema gari inakuja na technology ya “common rail injection” maana yake haswa nini nini? Yani ni kuwa inaboreshwa uchomaji wa mafuta na ulaji unakuwa chini? Pia hii common rail injection inapatikana kwa gari za Petrol ?
Hapo zamani kulikuwa na injector pump pamoja na mechanical nozzle kwa ajili ya diesel automisation, injector ilikuwa inafungwa kwenye flywheel , na ilikuwa pia ina ratibu timming za uchomaji , (firing order) moja ya disadvantage ya mfumo wa injector pump ni kuwa kwa sababu ipo connected kwenye flywheel, engine inapobeba mzigo hupungua speed, bayo pia hupunguza speed ya pump, ambayp nayo pia hupunguza speed ya nozzle atomization, kuna chain reaction flani ambayo huathiri perfomance once engine inapobeba mizigo, disadvantage ya pili ni kuwa injector pump haikuwa na pressure kali kwa ajili ya fuel atomisation, the best injector ilikuwa inatoa around 600 to 700 presseure bar. Hizi ndo zile zama diesel engine zilikuwa doggy slow na moshi wa kutosha
Common rail sasa ni mfumo tofauti, hapa kuna electronically conntroled fuel pump, kazi ya hii pump ni kujaza mafuta kwenye rail yakiwa katika pressure ya hadi 2000bar, neno common limetumika kwa kuwa nozzles , sasa zote huchukua mafuta yakiwa kwenye rail na yakiwa na pressure kali na preszurre sawa bila mpangilio wowote ,( firing order), kazi ya kutatibu mafuta kwenye common rail.hufanywa na sensors zilizopo kwenye flywheel, bazo hupeleka positions ya flywheel kwenye computer (ecu ) ambayo yenyewe sasa huzipa nozzles signal ya kuruhusu atomisation , moja ya advantage za mfumo huu ni kuwa speed ya flywheel haiaffect pressure kama kwenye injector pump. , pili mafuta yanakuwa atomosed kwa pressure kali kuliko injector pump , which allows better atomisation ana hence fuel economy, tatu hakuna makelele ya injector pump, nne kwa kuwa nozzle zinakuwa na mafuta tayari hadi shingoni , timming period na reaction time ni very rapid kuliko mechanical pump., nne tofauti na enjector pump ambayo ilikuwa ni mzigo constant, electonicaly contolled pump huwa haiwi on muda wote , kama pressure kwenye common rail ipo mahala pake hii pump huwa inakuwa disengaged na kupunguza mzigo wa engine .
Ndio sababu engine zinazotumia mfumo wa common rail huwa smooth , very silent and super powerful.