Namna ya kuweza kuishi DAR; Ishi kibepari

Dahh.. uko vizur taikoooon, hyo uki appy popote lazima utoboe, kaa kijanja.
 
Anza kutembelea watu ni muhimu Ujue kuna kuugua na kufiwa usije ukajikuta huna msaada, mifano ipo mingi.
 
Dsm kilichonishinda ni watu wake..waongeaji sana na wengi weupe sana kichwani ila maneno mdomoni pomoni..ndio mana wengi ni madalali..nenda k.koo,karume,masoko ya mazao,njoo kwenye viwanja na nyumba za kuishi yani bongo kila sehemu kuna madalali hadi kupata malaya wamejaa madalali..hichi kitu kinaniboa sana kwakweli.

Kingine ni ushabiki wa simba na yanga..yani kila kijiwe ni hayo tu ukizingatia wengine mpira ndio ulishatupita pembeni yani kukaa vijiweni naboreka kinyama bora nikae zangu home nizame jf mana ndio sehemu pekee naweza kukutana na watu wenye mind na utashi kama wangu.

All in all dsm ni sehemu rahisi sana kuishi kama una harakati zako..haliya hewa iko poa pia..na bidhaa yoyote unayotaka utaipata..viwanja na bata za maana utazipata hapa..makongamano semina na warsha mbalimbali zinafanyika hapa.

#MaendeleoHayanaChama
 

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

DSM ujanja ujanja mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…