Nampa pole sana Christian Ronaldo

Nampa pole sana Christian Ronaldo

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
"CIRO IMMOBILE" ANAVYOMNYIMA PUMZI "CRISTIANO RONALDO."
---------------------------------------------

Pale Seria A. Makipa wanapoiona jezi no 17 kwenye kikosi cha Lazio. Huwa wanaanza kusali sala ya salamu Maria na baba yetu uliye mbingni. Mwenye hiyo jezi anapoingia uwanjani. Nyavu huwa zinajua muda wa mateso ya Golgota umewadia. Na hata glove's za makipa wa timu pinzani, huwa zinaanza kufanya maombolezo.

Namuongelea kiumbe ambaye anaichezea timu ya Lazio. Kiumbe ambaye baada ya maji ya ubatizo kugusa kichwa chake. Akaitwa "Ciro Immobile. Huyu kiumbe leo ameweka hat trick. Lazio wameshinda goal 5-1 dhidi ya Sampdoria.

Ciro Immobile yupo kwenye kiwango cha moto mno. Na anamnyima pumzi vilivyo kaka yetu Cristiano Ronaldo. Bahati mbaya yeye ni shujaha asiyeimbwa. Waandishi wenye mioyo inayoshea D.N.A na shetani wanaamini. Kuipa utukufu miguu ya "Immobile" nisawa nakukosea adabu muda. Hawana habari naye.

Hawapo sahihi, wanaitenda dhambi ambayo kesho itawakosesha tiketi ya kupita mlango wa pepo."

Baada ya hat trick ya leo "Ciro Immobile" amefikisha goal 23 pale seria A. Goa 23 katika mechi 19 tu. Goal nyingi kuliko mtu yoyote katika ligi 5 bora za bara la ulaya. Kwa pale Seria A wanaomfukuza ni Romelu Lukaku wa Intermilan na Cristiano Ronaldo wa Juventus. Wote hawa wana vyuma 14. Immobile kawazidi vyuma 9.

Ronaldo na Lukaku wanaweza kumfikia. Lakini nikama wataungana na kufanya maombi ya siri. Immobile apate majeraha yatayomuweka nje msimu mzima. Akose mechi 19 zilizobaki.

Mwanaume "Ciro Immobile" February 20th atakuwa anafanya birthday ya kutimiza miaka 30. Tangu alipozaliwa kwenye mji ambao Ni paradiso ya watukutu. Mji inakopatikana ikulu ya maboss wa mafia. Mji ambao cocaine na Heroine zinauzwa kiholela tu kama sigara za sport kwenye viosk vya manzese. Naungelea mji wa Napoli Italy. Ciro Immobile alizaliwa mji wa Napoli.

Huu ukatili anaozitendea nyavu za Seria A msimu huu. Ni mdogo sana kulinganisha na matukio yanayotendeka kwenye mji kilikofukiwa kitovu chake.

Kwa wale wasiojua. Ciro alilelewa kwenye academy ya Juventus. Mwaka 2009-2012 alipandishwa timu ya wakubwa. Lakini alifanikiwa kuichezea Juventus mechi tatu tu. Baada ya hapo akaanza maisha ya kuzurura timu tofauti duniani kwa mkopo.

Sababu ya kutolewa kwa mkopo mara nyingi ni nini?! Sababu ni nyepesi kuliko tishu tunayoitumia kujifutia mdomo harusini. Pale tunapomaliza ukatili wa kuitafuna minofu ya kuku. Miguu ya Ciro ilikuwa haijaiva kimbinu. Hakukuwa na miujiza yakuogopesha magolikipa chini ya nyayo za miguu anayoimiliki. Jezi ya Juventus ilikuwa nzito kuliko mifupa inayounda uti wa mgongo wake.

Hii ndio sababu ya kutolewa kwa mkopo mara nyingi timu tofauti. Mwaka 2013 Ciro alikuwa Genoa. Mwaka 2014 alikuwa Torino. Mwaka 2015 alikuwa Borusia Dortmund. Mwaka 2016 alikuwa Sevilla. Alicheza nusu msimu akaenda tena kwa mkopo mwingine Torino. Baada ya hapo Lazio wakamnunua jumla.

Ameichezea lazio mechi 124 na ameifungia goal 90. Hii ikiwemo na hat trick ya leo.

Huu msimu huyu mwamba yupo moto mno. Na nafikiri waitaliano hawataki kabisa Cristiano Ronaldo aondoke Seria A na record ya ufungaji bora kwenye ligi yao.

Maana msimu uliopita mfungaji bora wa Seria A alikuwa babu Quagriallela. Alichukua ufungaji bora akiwa na jezi ya Sampdoria. Huku hati yake ya kusafiria ikimuonyesha ana umri wa miaka 36. Baada ya msimu huu ubora kuipigia filimbi ya offside miguu ya Babu Quagriallela.

Ameibuka kiumbe mwingine Seria A. Kiumbe ambaye licha ya ubora wake kwenye ligi yenye Cristiano Ronaldo, Alex Sanchez, Romelu Lukaku. Lakini bado kalamu za waandishi wa habari hazitaki urafiki naye. Ciro yupo kwenye kiwango safi kuliko boxer ya mzinzi anayesubiri promise ya kuzini. Na ninafikiri kuna maombi ya siri huwa yanafanyika Vatcan.

Kuiombea miguu yake isipate hitilafu. Ili akibakishe kiatu cha ufungaji bora kwenye ardhi ya Italy."

Nampa pole sana Christian Ronaldo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilijua lazima mambo yamuendee kombo yule mpenda sifa. Wakati mwenzake anaweka legacy ya ukweli pale Catalunya ili hata akistaafu awe mmoja wa ma-legend, jamaa mpenda sifa za kijinga yeye akaona eti aweke historia ya kucheza ligi nyingi, ujinga tupu.
 
1579498396539.gif
 
Binafsi huwa nawaona watu wanajifanya mashabiki misukule wa kitu chochote hawana akili
 
Kwa hiyo? hivi wewe na kabila lako mkienda kwake Ronaldo hujui anaweza kuwalisha mpaka maisha yenu? Una nini mpaka umponde wewe na kabila lako?
 
Back
Top Bottom