Nampenda huyu dada,lakini ananikatisha tamaa!nifanyaje mie??

Nampenda huyu dada,lakini ananikatisha tamaa!nifanyaje mie??

Man Ngosha

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2012
Posts
219
Reaction score
69
Habari zenu wanaJF,
Mie nimekuwa katika kutafuta mwenzi wa maisha muda mrefu,na kuna wakati nilikata tamaa baada ya kuwa kila ninayempa proposal yangu anadai yuko na mtu wake.
Sasa,wiki mbili zilizopita nimekutana na mdada ambaye kiukweli ninampenda sana kwani ana sifa zote nitakazo mie,kwa hiyo nikaanzisha mawasiliano naye na mwisho wa siku tukapanga kukutana ili nimweleze hitaji langu.Baada ya kumweleza yangu ya moyoni,alidai yeye hataki kusikia habari ya uhusiano wa kimapenzi kwa sasa kwani AMEACHANA NA MPENZI WAKE MWEZI JANUARY 2013 baada ya kuwa katika mahusiano tangu akiwa form one.Baada ya kusikia kuwa ameachika nilifurahi sana sababu nilijua hii ndo nafasi yangu,japo alisema hataki mapenzi tena labda urafiki wa kawaida tu,mi sikuona taabu nilimwambia nimpe muda afikirie kwanza ombi langu!!
Tangu wakati huo nimekuwa nikionesha ukaribu naye sana,ikiwemo kumjari na kumpa zawadi LAKINI Amekuwa akinambia NAPOTEZA MUDA WANGU TU,
SASA Wadau,naombeni mnishauri mwenzenu nifanye nini ili huyu dada awe wangu wa maisha?Nampenda kwa moyo wangu wote na nataka aje awe mama watoto wangu!NIFANYEJE JAMANI???
 
Mwenzio kasha kata tamaa, hawezi amini wanaume. Kwaiyo vizuri kakuambia wazi na ukweli.
Hapo ni kama game kaka angu. Utaishi bila uhakika.

Piga kimya, atakutafuta, nawe mwambie kavu hautaki kuchezeana upo serious, na utakuwa unaumia kumuona face yake bila kuwa nae
 
Yan mkuu unavyoeleza nami npo kwenye wakati mgumu kama ww
 
Dah,nataman angeniamini ninachomwambia!Nikimcall anapokea tu vizuri,nikianza kuongelea mapenzi anakata simu!
 
Dah,nataman angeniamini ninachomwambia!Nikimcall anapokea tu vizuri,nikianza kuongelea mapenzi anakata simu!

she must have been hurt badly.mpe time.....kuwa rafiki yake wa kawaida....muwe mnaenda outings na kuongea mambo kama rafiki baadae atakuwa 'amekujua' hivyo ukimtokea atakuamini:confused2:
 
Mpe mda tu huyo coz kashatendwa mda si mrefu bado ajasahau, we mfanye kama rafiki tu kw sasa mpaka akujui vizur atakubali tu.
 
Sasa kama hakutaki kwanini kulazimisha? Baadaye akikuingiza kwenye matatizo utamlaumu binti wa watu wakati amekupa ukweli lakini wewe hutaki kuupokea? Kwani duniani yeye tu au nawe una tatizo unaloficha?
 
Sasa kama hakutaki kwanini kulazimisha? Baadaye akikuingiza kwenye matatizo utamlaumu binti wa watu wakati amekupa ukweli lakini wewe hutaki kuupokea? Kwani duniani yeye tu au nawe una tatizo unaloficha?

mie nahisi hajatueleza yote,kwa nini wote wanawake wamkatae?...kuna wanaloliona ila yeye halioni....labda aanze kujichunguza mwenyewe.....:confused2:
 
Dah,nataman angeniamini ninachomwambia!Nikimcall anapokea tu vizuri,nikianza kuongelea mapenzi anakata simu!
Ngosha, mlango mmoja ukifungwa, mingine mingi inakuwa wazi. Huo umefungwa, tafuta ulio wazi. Kwa nini unataka kulazimisha funguo za Solex zifungue kwenye kitasa cha Union?
 
Mi sina tatizo lolote,wasichana ninakutana nao ni wengi,lakini si wote wanafaa kuwa wenzi wa maisha yangu!Unapotafuta mwenzi wa maisha,unapaswa kuwa makini si kila msichana anafaa!Katika kufanya systematic selection,ndo nikakutana na huyu aliyeachwa!Nashukuru kwa idea ya kuwa karibu naye kwanza kama rafiki ili anifahamu vizuri
 
Kama ulivosema kua huyo dada ametoka kuachana na mtu wake, inawezekana aliumizwa sana, hivo anaogopa mahusiano kwa sasa, mpe muda wa yeye kukuamini, kwa kua kinachomsumbua ni hisia za kuumizwa na anahisi labda wewe ni walewale, sasa unapokua kama unamlazimisha ndio kabisaa anakuona kama hufai na unazidi kumtisha, Jenga urafiki wa kawaida kwa sasa ili aweze kukujua walau kidogo, usimgusie mambo ya mapenzi, hata mkitoka out epuka kuonesha kua una haraka ya kuwa nae.
 
Asante lateni,
Ushauri wako una mantiki sana!!nitaufanyia kazi
 
Kama aliyemuacha hajaoa lazima amrudie so muulize, akikwambia aliyemuacha kaoa mtu mwingine basi komaa...
 
Nashukuru wadau kwa michango yenu ya kujenga,naahidi kuzingatia ushauri wenu!!!
 
nenda nae taratibu tu atanasa mtego usikate tamaa
 
vumilia atakubali bado anamawazo mengi juu ya yaliyomkuta
 
We tulia bana,hata kuku anataga then analalia 21 days then anatotoa,tofauti na hapo atakuwa wakichina
 
Back
Top Bottom