Kabla hujachukua hatua yoyote, jaribu kumjua kidogo - kama yuko single au tayari ana wake. Hii itakusaidia sana. Ingawa kimaadili "IMEKATAZWA - Msitongoze walimu wenu", ikiwa una uso usio haya unaweza kujaribu bahati yako. Lakini ukielewa kuwa ana wake, kwanza heshimu uhusuano wake na usijiingize, pili usitarajie kupata jawabu la kuridhisha.
ANGALIZO: Sote kwa wakati mmoja au mwengine tulipokuwa adolecents tumewahi kuwa na hisia kama hizo kwa walimu wetu (he&she), lakini uzoefu unaonesha mapenzi ya namna hii yanakaribia kuwa "Impossible Mission", sio kwa sababu ya viwango vyenu vya elimu, bali kwa sababu yeye ni mwalimu na wewe ni mwanafunzi. Kwa maneno mengine, kwa mwanafunzi wa kiume kumpenda na kufanikiwa kwa mwalimu wake (she) inakuwa shida kidogo, tafauti na walimu wa kiume kwa wasichana. Sikuvunji moyo lakini kwanza shughulika na masomo yako.