Nampenda ila katiwa mimba

Nampenda ila katiwa mimba

Kapepo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2015
Posts
1,066
Reaction score
1,194
Kuna msichana tumekuwa kwenye mahusiano tangu mwaka jana mwezi 11, ila kipindi chote icho hakuwa na imani na mimi kama nipo serious nae kwa sasa anadai ananipenda sana baada kugundua upendo wangu wa dhati kwake, tatizo linakuja kwa sasa ana ujauzito wa mwez mmoja kapachikwa na baharia mmoja huko buza na huyu binti kawaeleza ndugu zake ananipenda mimi na hataki kuwa na huyo baharia na jamaa hana mpango na iyo mimba,

nilichoamua kumwambia siwezi kuwa nae kwakua siwezi lea mtoto wa mtu pia nina safari ndefu katika maisha haya huyu binti hataki kunielewa kabisa ukweli ni kwamba nilikuwa na marengo nae mazuri tu ila hii hari aliyonayo imenikatisha mood kabisa ila yeye hataki kunielewa kwakweli nimejaribu kumsihi alee mimba yake na mchizi anadai anataka kuitoa hiyo mimba ili awe namimi nije kumuoa ukweli nipo njia panda sijui nawezaje kuishinda mtihani huu ukizingatia wazazi wake wamemkataza hasitoe hiyo mimba na huyu binti hataki kuelewa yeye anataka kuwa namimi na mimi siwezi lea mtoto wa jamaa kwa kweli nampenda sana ila huu mtihani umeninyima nguvu sijui nini nifanye
 
Umetaja kweli nyingi na mojawapo ni ukweli huwezi kuwa nae, ukweli unampenda, ukweli kapewa mimba, ukweli anakupenda. Wewe ushasema huwezi kuwa naye maana ana mimba isiyo yako sasa sisi tufanye nini tena. Sikiliza moyo wako unataka nini, hakikisha una msimamo na unachokitaka hata ukiuliza au kuomba msaada watu wakupe experience au mawazo yao.
 
tatizo msimamo wake kutoa hiyo mimba ndio inanipa hofu ikitokea sijaoa familia yake na yeye watanichukuliaje mkuu ka si kurogwa nini kinafuata
 
Nimependa hapo ulipomuambia eti umetaja 'kweli nyingi'..!!

Hivi kumbe 'baharia wa buza' wako serious kwa kiwango hicho? Kapepo ulikuwa wapi eti mpaka mrembo wako anawahiwa kizembe namna hiyo??

Enwei, wanaume wa sasa sijui mnakwama wapi, maamuzi ni kitu mmeshindwa kufanya kabisa na ndiyo maana wanawake washajua udhaifu wenu wanacheza mno na akili 'zenyu'..!

Wewe ni mwanaume hupaswi kuongozwa na hisia kama sisi, unapaswa utumie zaidi akili yako kufanya maamuzi, Ni kweli unampenda, ilikuwaje aingie kwenye mahusiano na mwanaume mwingine wakati tayari ulikuwa naye?

'Once a cheater, always a cheater', mwisho wa siku mapenzi hayashauriki, fuata tu moyo wako Mr. Kapepo.!
 
shukrani kuu ntazingatia ushauri
 
Umetaja kweli nyingi na mojawapo ni ukweli huwezi kuwa nae, ukweli unampenda, ukweli kapewa mimba, ukweli anakupenda. Wewe ushasema huwezi kuwa naye maana ana mimba isiyo yako sasa sisi tufanye nini tena. Sikiliza moyo wako unataka nini, hakikisha una msimamo na unachokitaka hata ukiuliza au kuomba msaada watu wakupe experience au mawazo yao.
Asante kwa hii summary.
Nimeangalia post aliyoweka OP nikagundua hajaweka nukta hata moja. Kisha kichwa kikaanza kuuma.
 
Yaani hadi ilo unauliza yaani baharia ashakuchapia bado unashindwa ufanyaje mkuu tayari ushatengenezwa tayari usharogwa [emoji16]

Inauma ila we alikufanya "second option" ndo maana aka Ku cheat akupendi kivile ye anaangalia kwenye unafuu na ameku cheat na hana option nyengine mshikaj kamkataa kaamua arud kwako boya mwenye huruma

Unatia aibu hili si lakuomba ushauri kabisa

HIVI INAKUAJE SIKU HIZI WANAUME TUNASHINDWA KUFANYA MAAMUZI KWENYE MAMBO MADOGO KAMA HAYA HIVI SHIDA NI NINI WAKUU ?

we familia yake na wewe inakuhusu nini ? Piga chini hoe huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeongea point moja nzito sana.
Mleta mada alikuwa second option na yenye uhakika kiasi kwamba binti amejua kimbilio liko wapi.
Mtoa mada anampenda huyo binti ndo maana ametaja kweli nyingi, angekuwa hampendi angekuja kutupa mkasa tu na kutuambia alichofanya lakini yeye kaja kuomba ushauri.
 
tatizo msimamo wake kutoa hiyo mimba ndio inanipa hofu ikitokea sijaoa familia yake na yeye watanichukuliaje mkuu ka si kurogwa nini kinafuata
Wewe una maamuzi gani. Hapa naona unataka kudate nae lakini unaogopa baadae unaweza usimuoe. Na pia unaogopa usirogwe endapo ukifanya kumtenda, nahisi una uwezekano mkubwa wa kumuacha baadae kulingana na maelezo yako.
Kwa sasa unataka utake advantage ya kuwa kaachwa.Anaweza akakupenda au ataendelea kukuchukulia poa tu.
Mara nyingine second option ndo best option, mimi sina ushauri katika mapenzi kwakuwa pia siombi ushauri. Nikisikiliza akili yangu, moyo wangu, hisia zangu nikachanganya na uhalisia nafanya maamuzi. Kingine sina uzoefu katika mapenzi.
 
Hapo hakuna UPENDO hata 10% huo ambao umeupa thamani ya ukweli kutoka kwako wala kwake, sababu;

1. Mahusiano mmeanza NoV 19, means mpo kwenye uhusiano kwa miezi 4 tu.

2. Ndani ya Miezi 4, mwezi 1 tayari kashapewa mimba na Mchizi wa Buza.

3. Ndani ya miezi 4, wazazi wa binti washajua kila kitu na kuingilia.

4. Mwezi mmoja ni mimba changa sanaa, ambayo sidhani kama inaweza chelewesha maamuzi kwa muda wote huo.

Iko hivi kwa Mwanaume ( Mwanaume hasa) si swala la kumwambia hata jirani yako kua unaitaji ushauri, kwasababu hata wewe mwenyewe ujui nini unataka.

Jamii; Naomba mfahamu sisi wanaume hatuko hivi na hatujawah kua hivi, moja kati ya wanaume washamba wanatuchafua thamani yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na sijui anatoa ujasiri wapi wa kukubali kuwa second option
Mkuu umeongea point moja nzito sana.
Mleta mada alikuwa second option na yenye uhakika kiasi kwamba binti amejua kimbilio liko wapi.
Mtoa mada anampenda huyo binti ndo maana ametaja kweli nyingi, angekuwa hampendi angekuja kutupa mkasa tu na kutuambia alichofanya lakini yeye kaja kuomba ushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu mwaka jana mwezi wa kumi na moja tayari mshafikishana kwa wazazi, mshatambulishana na tayari ana mimba ya mwezi mmoja ya baharia wa buza.
 
Anachosema kamwambia jamaa mimba imeharibika kwahiyo atajifungua vizuri tu alafu mtoto atalelewa na wazazi wake ili mimi niendelee nae nimuoe jamani mimi nisije rogwa tu huyu mtoto hataki kuniacha tena na kaapa haniachi
 
Back
Top Bottom