Nampenda Lakini...??

Nampenda Lakini...??

Kinachoshangaza unakuta kwa miaka 15 baadae huyu mwanamke anaendelea kuua watu na mizimu yake duu🤮🤮
 
Kuna mdada ambaye nimempenda sana na ningependa awe wa kufa na kuzikana kama mambo yangekuwa yapo ndivyo sivyo, mdada ni mfanyakazi anaposition nzuri tu na anajiweza kimaisha,
kwa muda wa mwaka mmoja sasa nimekuwa na mawasiliano katika kipindi chote hicho hatujafanya wala kuvunja amri ya sita ila romance tumefanya,

nilitaka kujua historia yake kwa ufupi na aliniweka bayana kwamba yeye ana mtoto wa kike(4) ambaye alizaa na mume wa mtu na anavyodai alikuwa anampenda vizuri na kumtimizia mahitaji yake kama nyumba ndogo yake, nikapenda kujua ni kwa nini ameachana na huyo mtu ambaye ni mume wa mtu na anadai kwamba anampenda na wameridhika? akanambia ukweli kwamba huyo mtu alifariki kwa ajali ya gari akavunjika kiuno toka mtoto wao akiwa na umri wa miaka miwili,

Sikuishia hapo kwa sababu kama nilivyosema ni mtu ambaye anaweza/angeweza kuwa mke nikaona niendelee na maswali namshukuru pia alinijibu bila kuskip kipengele hata kimoja, nilimuuliza wewe najua ni mdada mzuri na unamvuto hivyo kwa miaka miwili ambayo umekaa bila huyo mtu wako (marehem) ni wazi kwamba unamtu/unatarajia kuwa na mtu mwingine mdada akanijibu ni kweli nilikuwa naye lakini distance zilitupa shida hivyo tukashindwa kuendelea (jamaa alikuwa anakaa Dar yeye Moshi) hapa aliskip some vipengelez...

katika pilika pilika zangu za kila siku nilikuwa mwanza nikawa nimefikia hotel moja mwanza nikapenda kula samaki tu maana sato niliwamiss kimtindo nikasema nikipata samaki na the lite castle burudaaaani kabisa .. nikaenda mwaloni kuna bar moja wanasamaki wazuri sana watu walikuwa wengi na nikajiatach kwenye meza ambayo kulikuwa na mbaba mmoja like 46yrs hivi .. nae alikuwa anajiburudisha na serengeti bariiiid nikaona kampani imekuwa nzuri sasa tukaanza kuchati nikamwambia mie nimatokea sehm fulani na ninafanya kazi huko ..akanambia kijana hata mie nilishafanya kazi kwenye huo mkoa na bahati nzuri alitaja kuwa ameshafanya kwenye hiyo taasisi ambayo mchumba/mke mtarajiwa anafanya kazi.

As a gentleman nikamwambia tu pale nina mchumba ambaye nataka Mungu akitujaalia tufunge ndoa
uzuri anamfahamu huyo dada alikaa kimya mwa muda kidogo yaani hali flani kama anataka kupotezea storry akaanza kunipa story zingine za kuwa ametoka kakola (Kahama mining huko) aah! nikaona huyu vipi mbona tulikuwa kwenye line moja lakini ananitoa tena? nikaona isiwe tabu bado tunapiga mtungi kidogo kidogo nitamrejesha tu kwenye reli huyu..

nikaanzisha story tena kwa swali la kizushi bro vipi hutaki niingie kwenye chama cha mavuvuzela? (waliioa na kuolewa) akacheka kidogo then akasema bwana mdogo ngoja nikwambia kuona ni vizuri sana lakini unatakiwa uchunguze niwapi unakwena kuoa akaleta mfano ule wa mababu zetu ambao walikuwa ukitaka kuoa wazazi ndo wanchukua jukumu la kuichunguza hiyo familia unakotaka kwenda kuoa, na walikuwa na maana yao kwa sababu kama familia ina historia ya ukoma watakwambia ...lakini kwa kizazi chenu mambo yamebadilika sana hivyo muwe makini sana..

Alinipa ukweli wa huyo dada kwamba kila mwanaume anayemtokea na wanakuwa katika mahusiano mazuri huyo mwanaume anakufa na mbaya zaidi wote wanakufa kwa kuvunjika viuno wameshakufa wanaume watatu hadi sasa kwa ajali za gari na wanavunjika viuno, kama unakumbuka huyo dada alishawahi kuniambia huyo aliyezaa nae amefariki kwa ajali ya gari na huyo wa pili kulingana na huyu brother amefariki kwa ajali pia na watatu nae kafariki kwa ajali pia ...

Mnishauri wanajamii mie kiuno changu nadhani bado nakihitaji na nipo kidogo confused kwa sababu mdada nampenda ila ninataka kumuuliza ukweli wote kama atakuwa yupo tayari kuniambia A-Z maana hizi pingu za maisha ambazo mnafungwa ni noma mazee...sio za kuingia kichwa kichwa..

Asanteni
Dah! Leo ni member wa 4 nakutana nae akiwa amefariki 😲 kwangu kuna usalama kweli?
 
Umeota nini usiku wa jana?
Mwewe kabeba kuku Hadi juu kabisa baadae mwewe akashuka bandani Tena na yule kuku kumbe juu ya mwewe kulikua na jogoo Tena!yaani kuku kwa chini jike halafu jogoo juu ya mgongo wa mwewe!nikamuona wife anatoka kwenda kucheki! Nikashtuka!!
 
Back
Top Bottom