Tunaposema mpole na mkorofi tunakusudia nani?
Yule anayekubali au kukataa kwa sababu VS yule anayebisha kila kitu (hambiliki)?
Yule anaye "reason" kabla ya kuamua au kufungua mdomo wake VS yule anayependa kusikia sauti yake kabla ya kusikiliza ya mwenzake?
Yule aliye na huruma, anayekuheshimu na kuheshimu mahusiano yenu, anayejali, anayekiri akikosea, anayejua kusema Asante, Samahani, Tafadhali VS yule asiyejali, asiyekuheshimu, anayejua kila kitu, majivuno na daima yuko "right"?
Yule anayependa kila kitu kizungumzwe na kufikia suluhisho VS yule ambaye neno lake ni sheria na maamuzi yake hayapingwi?
Bila ya shaka, yule awaye mpole kupindukia huyu huwa si upole bali zoba
Na yule awaye mkorofi kupita kiasi, huo si ukorofi bali ujinga (kwa maana pana ya neno lenyewe)