Nampenda sana Hoyce Temu, naipenda roho yake

Nampenda sana Hoyce Temu, naipenda roho yake

Chakula ya wakubwa tu huyo Wewe..Kama unataka tukutajie listi hapa ya watu wake.
Usishobokee tu ovyo ovyo.
 
Binafsi napenda kazi yake na hayo mengine unayoyawaza wewe pia. Mwanamke kujitambua, roho safi, ukarimu, uzuri ni ziada tu. Hoyce popote pale ulipo naomba uje unishike mkono au hata kunipa busu la shavu roho yangu ipone. Nimeoa lakini sina raha, nakuwaza wewe tu kila kukicha.
Ha ha ha mkuu bana usinichekeshe. Ukarimu na roho safi ya mtu umeipimia kwenye Mimi na Tanzania? Tulia na mke wako
 
Habarini Wadau,

Sio siri huwa ninampenda sana Hoyce Temu aliyekuwa Miss Tanzania nafikiri wa mwaka 1999.

Huyu dada amekuwa akionesha roho safi na upendo wa dhati kabisa kwa wasiojiweza na hasa watoto.

Katika kipindi chake cha "Mimi na Tanzania" Huwa anawashika, anawakumbatia na kuwajali watoto wenye matatizo makubwa kiafya kama vile ni wakwake wa kuwazaa.

Pia huwa anasisitiza wachangiwe na kupatiwa misaada mbalimbali.

Sikuwahi kujua kuwa kuna wadada wa kichaga wana roho nzuri hivi kwajinsi wanavyosemwa humu.

Mungu akutunze Dada Hoyce Temu na azidi kukupa moyo wa huruma.


AAMIN.

Ukiusikia upande wake wa pili ( Side B ) unaweza ukatamani umchukie Milele labda pengine hadi mtakapoona ama Jehanam au Paradiso
Daah..kumbe na yeye ana mambo mengi tofauti na tunavyomfahamu wengi?

Tena ya hatari na ya kutisha kama siyo hata ya kusikitisha.
 
Back
Top Bottom