Nampenda sana lakini kila nikiwaza kulea watoto ambao sijawazaa moyo unakuwa mzito

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Habari kaka Magical power, nina umri wa miaka 33 Nina Mtoto mmoja, sielewi Mimi ni single au nijiteje kuna jamaa ambaye tumetokea kupendana kwa miezi nane sasa, ila tatizo nikuwa aliachana na mke wake na ana watoto watatu na huyu ex wake.

Nampenda sana lakini kila nikiwaza kulea watoto ambao sijawazaa moyo unakuwa mzito kuolewa naye mtu azae Mitoto 3 yote ikasumbue kichwa Mimi na ubaya kitoto chake Cha mwisho cha kike kinemfanana mama yake nikikaona najaa wivu nahuzunika sana.

Na Inavyosemekana kwamba mama wa hawa watoto ni mtu anayependa ugomvi sana.

Nahitaji ushauri nifanye nini kwa hili nampenda sana mwanamume?
 
fata jinsi moyo wako unavyokuelekeza
 
Ninachokiona kwako ni ubinafsi. Wewe mwenyewe una mtoto ambaye siyo wake, halafu unasema hauko tayari kulea hao wengine. Sijakuelewa kwa kweli
 
Achana naye huyo mwanaume Dadaangu..
Kuhangaika kufuta vinyesi watoto wa watu haihusu kwa kweli..
Na huyu Bwana tia block kabisa asikuzoee..
Kwanza kwani ni lazima kuolewa eti?
 
Wewe una roho mbaya, huwezi kuishi na watu, leo huyo mwanao peke yako. Hutaki kulea wa mwingine ila unataka wa kwako alelewe
 
Achana naye huyo mwanaume Dadaangu..
Kuhangaika kufuta vinyesi watoto wa watu haihusu kwa kweli..
Na huyu Bwana tia block kabisa asikuzoee..
Kwanza kwani ni lazima kuolewa eti?
Kunleki 😝😝 kwaiyo ila uyo bwana kulea kijusi ambacho sio chake ni sawa et
 
Wala usiolewe, Lea mwanao. Utaenda kuchuma dhambi tu. Binafsi siwezi Lea mtoto wa mwanaume anayenikula hapana
 
Mmh kinachoshangaza hata ww ni mama wa mtoto achana na huyo mkaka usije ukatesa watoto wake bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…