Nampenda sana Relief Mirzska

kawther

Member
Joined
Dec 26, 2018
Posts
42
Reaction score
55
Najua wapo watakaoniona malaya, ila bora niseme liwalo na liwe.

Sababu za mimi kufungua ID mpya ni kwamba nkitumia ID yangu ya zamani bwana wangu atajua kuhusu hili. Na sina uhakika kuhusu huyu Relief Mirzska maana namuona tu alivyo na kasi hizi siku za karibuni.

Kiukweli mimi nampenda sana huyu kaka na natamani niwe nae, nimepitia thread zake najua ameoa ila nipo tayar vyovyote iwavyo na iwe. Jamani msinione malaya na msiniulize nampendea nini. Moyo ukipenda hula nyama mbichi, napenda anavyoandika, napenda kusoma English yake, mimi ni rafiki yake ila naona amekuwa mgumu kuelewa. Saa nyengine anaringaaa, ovyooo!!!

Kuna wadada humu kila anachopost wao wana-like tu, jamani wengine mnatuumiza na ndio maana nimeamua kuja hapa. Wadau hebu naombeni msaada wenu, shemeji yenu kila nkimwambia mimi sipendi anywe pombe hataki kuacha mpaka namchukia sasa na nadhani naingia kwenye penzi na Relief Mirzska ndio maana moyo wangu unamchukia huyu jamaa.

Kwani mtu raha si unatakiwa ujipe mwenyewe??

Na wewe Relief Mirzska punguza kuringa, mimi nipo tayar tupige shoo moja ya kibabe moyo wangu utatulia. Najua ushanijua, tafadhali we mkaka jamani aggghhhh.
 
Ngoja na mm nianze kulike comment labda nitampenda[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Maana si kwa mahaba hayo alafu wewe dada unaonekana ni Mgogo
Kwann umemfananisha na mgogo
Kwamba wanawake wakigogo ndo huwa wanafunguka juu ya hisia zao kwa wanaume au? Ungejazia nyama kidogo mkuu kuondoa maswali mengi. BTW hata mwanamke anahaki ya kupenda pia na kuelezea hisia zake juu ya yule anaempenda sema bas tu ilishazoeleka yy mpaka aanzwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…