Ndagullachrles
JF-Expert Member
- Jun 20, 2023
- 256
- 259
Kuna majina manne ya wabunge wa viti maalumu(ccm)mkoa wa Kilimanjaro ambayo wanatajwa sana kwenye mitandao ya kijamii kwamba watapasua tena katika kinyang'anyiro cha kura za maoni kupitia Umoja wa Wanawake wa Chama cha mapinduzi(UWT)na kuelendelea kupeperusha bedera ya CCM kwenye bunge lijalo la 13.
Hawa si wengine ni Shally Raymond,Esther Maleko,Zuena Bushiri na Ummy Ndeliananga ambaye ni Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu,sera,bunge na uratibu.
Lakini jana jumamosi juni 28,2025 baada ya chama cha mapinduzi(ccm)kufungua pazia la uchukuaji wa fomu za ubunge na udiwani,alijitokeza mwanamama Namrinji Mnzava "mwanamke wa shoka"akachukua fomu ya kuomba kuteuliwa na UWT kuwa mmoja wa wabunge wa Viti maalumu .
Namrinji ni kiongozi ndani ya chama akiwa na kofia mbili moja ni mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Same na pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Umoja wa wanawake wa ccm(UWT)mkoa wa Kilimanjaro.
Nafasi hizi mbili za uongozi ndani ya ccm zimemjengea uwezo wa kukijua chama vizuri akishirki shughuli mbali mbali za ujenzi wa chama na ndani ya UWT wanamfahamu vizuri hivyo hakuna shaka kwamba mambo yatakuwa ni moto kwenye kura za maoni .
Kazi kwenu wajumbe wa UWT kuchanganua na kuamua nani ni nani kwa wanaoomba kura zenu,wapimeni waliopita waulizeni kama wametekeleza viruzi ilani ya chama cha mapinduzi katika kipindi cha miaka mitano ya ubunge wao na kama hawajatekeleza ipasavyo basi tumieneo sanduku la kura kufanya uamuzi