Namshauri GSM avunje Mkataba na TFF ili Pesa Zitumike Katika Usajili Yanga SC

Namshauri GSM avunje Mkataba na TFF ili Pesa Zitumike Katika Usajili Yanga SC

Sio kwamba nimekuwa mshabiki wa GSM kuwekeza pesa kwenye Ligi badala ya kwenye Klabu.

Bali ninalipinga vikali kitendo hiko. Kwanini asiwekeze mpunga kweye usajili wa wachezaji katika dirisha lijalo...?

Kwanini apeleke pesa TFF ambayo mwisho wa siku itaenda kuwafaidisha wengineo..?

Mimi ninamshauri akae meza moja na TFF ndani ya siku chache ili mkataba uvunjwe, maana sisi wanajangwani tunamapungufu makubwa sana katika eneo la Kiungo pale. Hata maeneo mengine pia.


Maombi yangu ninajua wazi yatamfikia GHALIB maana nimetaarifiwa kuwa uncle wako yuko kwenye majukwaa ya michezo mitandaoni ili kukusanya intelijensia.

Ni Upuuzi kupoteza pesa ambayo inhetifaa kwenye usajili wa dirisha dogo kwenye vitu vya kipuuzi.

Inakadiriwa mahitaji ya usajili wa uboreshaji kikosi ktk dirisha dogo ni Bilioni 1.5.

Yasikie haya GSM, Achana na upuuzi wa kutawanya pesa.
Kuna mtu anapenda hasara miaka yote?!!..
 
Back
Top Bottom