Namshauri Malinzi ajiuzulu Urais wa TFF ili amalizane na Jamhuri

Nasema mwanzo mwanzoni kuwa mimi ni Mwanasheria na Wakili Msomi. Najua kuwa kutuhumiwa na kushtakiwa si kukutwa na hatia. Kila mshtakiwa si mwenye hatia hadi mahakama itamke hivyo. Mambo hayo,kama moja ya haki za msingi za binaadamu,nayajua na kuyaheshimu.

Rais wa TFF,Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu wake Mwesigwa wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya jinai mbalimbali yakiwemo ya kutakatisha fedha. Kabla ya hapo,Malinzi alikuwa moja ya waliochukua fomu za kugombea tena Urais wa TFF.

Ili kupunguza mzigo wa mambo na kukubali yaliyompata kimaisha,namshauri Jamal Malinzi ajiuzulu Urais wa TFF ili apate nafasi ya kumalizana na Jamhuri kwenye kesi yake ya jinai. Kuendelea kuwa Rais wa TFF akiwa mshtakiwa kunaweza kutafsirika kama kung'ang'ania kichaka chake cha 'kupiga dili'.

Kujiuzulu,pamoja na kupunguza mzigo,kutamfanya Malinzi awajibike ipasavyo kwa yaliyompata na kukubali kilichomkumba kimaisha. Hakuna haja ya Mshtakiwa kuendelea kuwa Rais wa TFF au hata kujadiliwa kama mgombea mtarajiwa wa Urais wa TFF. Apambane kwanza na jinai yake.Kujiuzulu,wakati mwingine,huilinda punje ya heshima iliyobaki!
Mramba alikataa kujiuzuru na kweli alipeta hadi mwisho.
Msuya alikataa na kusema labda aliyemteua amfukuze na baadaye akapewa kuwa waziri mkuu

Malinzi atang'angania hadi mwisho wa kesi. sisi ni wapuuzi tu!
 
Swali kubwa kwangu ninalojiuliza, ni hili.....

Kwa nini hii ishu iibuke wakati wakitaka kuingia kwenye uchaguzi ?

I doubt, kuwa..... these are Just politics of elections !!

Hakuna sababu ya kuachia ngazi kwani inawezekana 100% kuwa hii ni kesi ya kutengenezwa tu ili kumuondoa mtu ktk reli ya kutetea kiti chake cha uongozi/urais wa TFF....!!!
 
Nami namshauri aachie ngazi atashangaa mambo mengi kwenye ile kesi yatapungua nguvu!! Hata dhamana atapatiwa......akubali yaishe aachie ngazi FIFA hata wakija hawezi kumbadilishia ile charge sheet! Na kwa awamu hii wako tayari tufungiwe hata miaka 5 ila Ile kesi ipo pale pale!!!
Uzuri ni kwamba FIFA wanaona kuliko hata TAKUKURU , Simtaki Malinzi na nimeongoza kampeni humu jf ya kumng'oa , LAKINI KAMA KWENYE KESI HII KUNA UZUSHI , WALAANIWE WOTE WALIOTUNGA UOVU HUU , na ni Uhakika FIFA WATATUTANDIKA VIBAYA SANA !
 
Safi sana ukiwa mtu unayependa haki hukubaliani na figusi za namna hyo hata Mimi simtaki ila tumtoe kwa njia nyingine
 
Nasema mwanzo mwanzoni kuwa mimi ni Mwanasheria na Wakili Msomi. Najua kuwa kutuhumiwa na kushtakiwa si kukutwa na hatia. Kila mshtakiwa si mwenye hatia hadi mahakama itamke hivyo. Mambo hayo,kama moja ya haki za msingi za binaadamu,nayajua na kuyaheshimu.

Rais wa TFF,Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu wake Mwesigwa wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya jinai mbalimbali yakiwemo ya kutakatisha fedha. Kabla ya hapo,Malinzi alikuwa moja ya waliochukua fomu za kugombea tena Urais wa TFF.

Ili kupunguza mzigo wa mambo na kukubali yaliyompata kimaisha,namshauri Jamal Malinzi ajiuzulu Urais wa TFF ili apate nafasi ya kumalizana na Jamhuri kwenye kesi yake ya jinai. Kuendelea kuwa Rais wa TFF akiwa mshtakiwa kunaweza kutafsirika kama kung'ang'ania kichaka chake cha 'kupiga dili'.

Kujiuzulu,pamoja na kupunguza mzigo,kutamfanya Malinzi awajibike ipasavyo kwa yaliyompata na kukubali kilichomkumba kimaisha. Hakuna haja ya Mshtakiwa kuendelea kuwa Rais wa TFF au hata kujadiliwa kama mgombea mtarajiwa wa Urais wa TFF. Apambane kwanza na jinai yake.Kujiuzulu,wakati mwingine,huilinda punje ya heshima iliyobaki!
Ninakushauri uishauri jamhuri iache mara moja kuingilia TFF uhuru wake wa kuchagua viongozi wake
 
Kwahyo EL, chenge, rostam, and Co sio mafisadi? Maana mahakama haijawahi tamka
 
Back
Top Bottom