Namshauri Rais Samia afanye kitu kimoja kikubwa sana ili iwe 'statement' kwa wale wanaomsumbua

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Ni ukweli kwamba toka Rais Samia Hassan ameingia madarakani, ameona umuhimu wa kubadili muelekeo wa nchi katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Na ni ukweli pia kuwa kuna watu wanamvuta ili asifanye mabadiliko hayo maana yanaonekana kama ni fedheha na kejeli kwa mtangulizi wake.

Huu ni mkwamo mzito kwake na inaonyesha anahangaika kuupatia suluhu. Nadhani hatua za haraka na za makusudi inabidi kuchukuliwa ili aweze kutoka katika tope hili. Huu mkwamo unahitaji aggresive approach. Ni wazi kuwa kundi la Magufuli lililopo Bungeni wame test, wakaona ni kweli wana nguvu na wanaweza kutikisa kiberiti kikatikisika. Kwa jinsi wanavyoendelea kujijengea confidence, litakuwa ni kundi hatari ndani ya CCM na katika nchi. Akitokea kichaa mmoja wa kuwaongoza, kuna hatari kubwa iko mbele.

Njia pekee ya kulizima kundi hili ONCE AND FOR ALL, ni KUFANYA (siyo kusema) jambo moja kubwa litakaloonyesha kuwa nia yake yafuata maono anayotaka yeye, hakuna anayeweza kuizuia na halazimiki kufuata njia za mtangulizi wake. Asipofanya hivyo, hiki kiza kitamuandama hadi anamaliza kipindi chake (kama hawatamuangusha kabla) na hataweza kujenga legacy yake yoyote ya kukumbukwa. Pia kuna uwezekano kama hataonyesha aggressiveness sasa hivi na kulisambaratisha kundi hili, hiyo 2025 hawezi kupita hata ndani ya CCM.

Kwa hiyo ushauri wangu wa Rais Samia, fanya jambo kubwa litakaloonyesha kuwa wewe umeamua kutengeneza njia yako mwenyewe, hata kama jambo hilo litawaoffend baadhi ya watu. Usikubali kuyumbishwa au kushurutishwa kufuata njia za wengine, hao wanakwambia hivyo kwa 'maslahi' yao wenyewe ya kisiasa.
 
Ungedokeza hata tu ka ushauri afanye nini hasa ili kwa hilo ‘jambo kubwa’ litokee

Nafikiri una maana afanye maamuzi ili watu wamuogope labda kumfukuza mtu mkubwa humo serikalini wa kariba ya PM au?

Mwendazake katuharibu I see, yaani mpaka yatengenezwe matukio (Ubabe) ndo heshima ionekane.

Mie cha kumshauri afate katiba ya nchi na labda hiyo ilani ya chama chake (hata kama hiyo ilani kuna baadhi ni pumba tu ) lkn atakuwa na la kujitetea.
 
Kwa nini unaona kundi la JPM ni hatari kwa Samia? Wakati Samia mwenyewe anasema na kuamini katika ideology ya JPM for your info watu hatari ni anti JPM na wahuni wa mitandaoni wakiingozwa na Lissu na Wafuasi wake.
 
Ninachompendea huyu Mama yeye ametulia tu ana-buy time kwanza ku-secure uenyekiti, after then sasa 😀
 
Kwa nini unaona kundi la JPM ni hatari kwa Samia? Wkt Samia mwenyewe anasema na kuamini katika ideology ya JPM for your info watu hatari ni anti JPM na wahuni wa mitandaoni wakiingozwa na Lissu na Wafuasi wake.
Ndio linalalamika sana kuhusu Legasi legasi legasi linasahaua huyo legasi demander hayupo tena.
 
Haya anweza kufanya. Arudishe mchakato wa Katiba mpya ile ya warioba, apeleke muswaada wa kutunga sheria ya kuyapa dhamana makosa wote, awaachilie masheikh wa uamsho.
 
SSH ni dhaifu, period, alijaribu kuruhusu ujinga wa kujaribu kumchafua JPM kwa propaganda, ameona joto na mapigo yamekuwa makali amewaruka hao wachafuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…