Namshukuru Mungu JF imenipa mke mwema

Mbwa dume

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
5,934
Reaction score
10,206
Kuna kipindi nilikuja hapa jukwaani kulalamika na kuomba wanajukwaa hili wanisaidie kumpata mwanamke niliyempenda sana na ni member anayejulikana kwa jina la rubii baada ya jitihada za kumbembeleza akashindwa kabisa kunikubali pengine baada ya kujua biashara yangu ( kuuza na kusambaza majeneza, sanda na vifaa vyote vya kuzikia).

Nilitumia kila njia kumbembeleza pamoja na kuahidi kumwoa na kumpa kila atakachotaka lakini ilishindikana. Kama ujuavyo kila jambo hupangwa na Mungu, kuna member waliokuja Pm ili kutaka japo kunifariji.

Mwisho wa yote kuna mdada mmoja akavutiwa na mimi na kuanza mawasiliano ambapo baadae tulikubaliana kuonana nikamtumia nauli akaja Dom tukafahamiana she is naturally beauty na amekubaliana na maisha yangu na tuko katika maandalizi ya kwenda kweo kutoa posa.

Nimeamini kwamba sio kila mwanamke aliye JF ni malaya au mchunaji kuna wanawake wako serious kuolewa. Ningemtaja lakini kulingana na umaarufu wake hapa jukwaani sintomtaja mapema mpaka tukishafunga ndoa. Ana elimu nzuri na ni mwajiriwa serikalini na ameikubali kazi yangu.

Nawashukuru mods na waanzilishi wa JF pamoja na wote mlioniombea mema.
 
Dahh hongera mkuu... Dom unaish sehem gan?
 
[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji114] [emoji114] [emoji114]
 
Mbwa Dume kapata mbwa jike... Imetuliaaaa mamaaaaaaaaa... Twanga pepeta nambari waniii
 
Inahitaji ujasiri wa kitekaji kujilipua na mwanamke au mwanamke tena ukaamua kuoana nae huku mtandaoni
 
Reactions: BAK
Tatizo ni lipi Mkuu!? Kwani kuna tofauti gani kukutana na mpenzi humu mkaanza kupendana, hatimaye kukutana na kama wote mnakubaliana kwamba mko tayari kuishi kama mume na mke basi mkafunga pingu za maisha!?

Usilidharau penzi linaloanzia mtandaoni, lina majaribu kama penzi la wanaokutana vyuoni, maofisini, kitaa etc lakini pia linaweza kushamiri na ndoa kufungwa.

Hapa jamvini kuna wanaume na wanawake wenye sifa nyingi za kuwemo kwenye ndoa.

Inahitaji ujasiri wa kitekaji kujilipua na mwanamke au mwanamke tena ukaamua kuoana nae huku mtandaoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…