kwa kuangalia haraka haraka tuu, kama watu wengi wa humu ndiyo wamesoma udsm, kweli kazi ipo huko nyumbani.
Kama na wewe umesoma nje ya nchi, halafu unaandika kitu kama hiki basi ukirudi nchini itakuwa shida sana; pia huko uliko wanapata shida vile vile. Nasema hivi kwa sababu:
1. post yako ya kwanza ilibidi iwe utambulisho lakini wewe umerukia kuleta mada, tena kwenye jukwaa ambalo sio mahala pake;
2. hauna basis wala back up wala evidence yoyote ya thesis yako;
3. Unaonekana hauna uzalendo na nchi yako, ni sawa na wale ambao wanakiita Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Choo Kikuu au Chuo cha Manzese;
4. Hivi Tanzania haina vyuo vikuu vingine mbali na UDSM? Kwa nini usifanye utafiti kwa kuzingatia vigezo ulivyonavyo ili kufikia hiyo real conclusion yako badala ya kufikia the hanging one - ulikotokea hata hapaeleweki;
5. Unashindwa kuelewa kuwa mtu yoyote duniani anaweza kujiunga na community hii kwa sababu ni online na kwa uhakika zaidi ungeweza kuwaomba admin hiyo info kama rules zinakubali ili uweze kutengeneza hoja;
6. Huko ulaya na amerika na kwengineko pia kuna vyuo vya ajabu ajabu tu - mfano ni vyuo ambavyo havijawa accredited and registered; kwanza yawezekana wewe unasoma huko huku ukiogesha mizee ya kizungu au kusafisha vyombo hotelini au kusafisha vyumba vya hotelini ili upate pesa ya kujikimu na kujiona bora kuliko aliyesoma Tanzania hasa UDSM;
7. Kwanza unaijua system ya kutoa elimu UDSM? Kama ndio, je umeilinganisha kwanza na ya huko unakosoma au ulikosoma? Kama hapana, sasa unafikiaje hiyo conclusion yako?
Kwa kumalizia nafikiri shule/ chuo ulichosoma wewe ni cha ovyo au wewe mwenyewe ndio bongo lala. Naomba utuambie level yako ya elimu na ufaulu wake; halafu utuweke literary work hata moja uliyofanya kwenye taaluma yako - yaani dissertation au thesis au article yoyote uliyo-publish kwenye reputable peer reviewed international journal!!!