Namshukuru mungu sikusoma UDSM

TAFADHALI SANA nakusihi kwa paa na ayala wa angani usionyeshe ujinga kwenye forum kama hii ambayo imeitwa ya watu wenye uwezo wa kufikiri sana. Sidhani kama ulishirikisha ubongo wako wa ufahamu na hekima kutoa mada hii hewani. Nafahamu kua waliosoma na wanaoendelea kusoma katika chuo kikuu cha DAR ES SALAAM ni waungwana na wastarabu na wala hawata jihusisha na kujibu ujinga huo. Hilo sio jambo la KUMSHUKURU MUNGU KABISA nadhani katika fani uliyosoma kama kweli umesoma kati ya mapungufu makubwa uliyo yapata ni kuto pita katika mlima ule. POLE SANA najua unajutia kwa kua kama umesoma hivi vyuo vinavyo itwa vya kata ni kutokana na kufaulu kwako kwa kiwango kidogo.

Nna uhakika kabisa ulipo pata usaili katika chuo hicho ulichosoma au unachosoma ulisema tu haya ila hamu yako kubwa ilikua kupitia pale. samahani sana hebu jaribu kama kukosea uende kijijini useme unasoma chuo kikuu halafu jutaje hicho chuo chako cha kata ulichosoma kama watakuelewa. Tafadhali kama ni muungwana hata wa asilimia sufuri tutake radhi kwa kauli yako.
 

Kaka nimesoma UD lakini kwa sasa sipafagilii kama enzi hizo za 1990's. Naona sijui ni ukali wa maisha walimu wengi wamejitosa kwenye Consultancy zaidi na kuacha kufundisha. Watoto wamekuwa wanakalia masesa tu vitabu hawasomi. Naona chuo changu UD kinaenda kupoteza umakini wake na kupitwa na chuo kama Mzumbe. Vijana waliokuwa vipange enzi zetu tumaliza form six chaguo lilikuwa twende UD lakini kwa sasa naona vipanga wanaenda Mzumbe. Kuna kijana wa jirani yangu alimaliza form six mwaka juzi ana Division one ya point 4 kakataa kwenda UD kaenda Mzumbe, kumuuliza dogo imekuwaje anasema hapafagilii watu ni wengi madarasani ufundishaji emebaki kukomaa na madesa. Najiuliza kwa nini wachukuwe wanafunzi wengi kiasi hicho wakati vitendea kazi ni vichache? Madarasani vijana wanakaa wanapumliana kwenye shingo tu unatokwa jasho utafikili hauko darasani.

Nikaabatika kupata elimu ya wenzetu waliondelea nikaona ni kweli wanastahili kuitwa watu wa ulimwengu wa kwanza, upo darasani unafeel kweli unasoma, hakuna mwalimu mwenye degree ya pili /Masters anaruhusiwa kufundisha hata kutoa semina elekezi kwa watoto wa degree ya kwanza, lazima uwe na PhD na umeshapata uzoefu kwa mda. Sasa leo hii Chuo changu UDSM vijana wanamailiza degree ya pili bila uzoefu waliunga toka ya kwanza wengine wanapewa na vipindi kufundisha. Mapinduzu makubwa yanahitajika katika chuo mama UD Ili heshima iweze kurudi. Mwishoe chuo kinaweza kupitwa na vyuo vya CBE, IFM na Tumaini kama mabadiliko ya makusudi yasipofanyika.
 
Mbona kama Nancy umesema kitu hakijakamilika. Ni kweli kuna matatizo mengi sana UDSM.. Ila dawa sio kukimbia matatizo. Ni kuyarekebisha. Kwa bahati mbaya unasema ubaya wa UDSM kwa kuangalia majadiliano ya JF. Una uhakika watu wote waliomo humu ndani wamesoma UDSM?Siyo mchezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…