Namtabiria Shilole kuja kuwa msanii wa kike mwenye pesa ndefu kuliko wote

Kuna siku niko dar, nilienda pale ktk mgahawa wake block 41,mdada mjanja mjanja sana,akifanikiwa si shangai

Naona ktk picha hapo yuko na CEO Kindamba ,safi Sana ,napenda wadada wa hv ,sio wale akina.....

Wadada wa Tabora mapambano ya kutafuta hela wanajua pia

[emoji767]101-03-821.M|T|C
 

Hujakumbushia deni la pilipili...
 
Hivi huyo jamaa ni fundi gereji kabisa au ana miliki gereji?

ni fundi gereji , before hajaolewa na shilole nimeishi nae kitaa kimoja mwananyamala kwa mama zakari, geto langu kwa nyuma ndio alikua anakaa yeye na mke wake ( mama Anuari ) ambae kamuacha baada ya kua na shilole(dah umbea huu)

baada ya kuvishwa pete , akaama m/nyamala mazima!
 
Sipati picha kitu gani kilichowakutanisha fundi gereji na msanii star πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€...Hapo jamaa inabidi awe mtu wa mazoezi,puturu,mchuzi wa pweza ili aendelee kudumu kwenye kazi ya kuolewa.
 
sijui kwanini na Mimi najikuta nampenda huyu Dada mungu amsimamie katika shughuli zake
 
Daah kutoka Moyoni nampendaga sana huyu dada,hanaga mashauzi ya kif.ala fala anacheka na kila mtu,mbali na hapo akiamua kujichetua kutokana na muktadha wa kazi yake anajichetua kweli....God Bless shishi...hivi unajua kwa nini CMG huwa hawamuachagi kwenye tour za Fiesta?
 
Mimi pia nampenda sana, nilikuwa simuelewi mwanzoni ila baadaye nikaja kumuelewa ni mtu wa namna gani. Napenda alivyo social na kilamtu, pia she's real tofauti na wasanii wengine ambao most of them wanaishi maisha ya Tamthilia. Hata wasanii wenzake inaonesha wanampenda...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…