Namtafuta Babys Walker (Umri Miaka 5)

Namtafuta Babys Walker (Umri Miaka 5)

Wataalam habari zenu.

Kuna mtoto anashida ya kutembea, mara ya kwanza alikuwa hawezi kukaa, alikuwa analala tu. Tukamtafutia baby seater.
Sasa anakata, Sasa ni wakati wa kumtafutia baby walker. Naamini atasimama na kutembea.

Naona nguvu anazo ila kuna shida za hapa na pale za kiafa. Ikiwemo kuongea hawezi ila anasikia na anaweza kuongea mambo anayojisikia.

Nitapata wapi baby walker ya Umri huo? Hata kama ni ya kuchonga. Mfanano na hii ama zinginezo.
Pole sana na hongera kwa kumjali sana mwanao, endelea hivyo hivyo usimkatie tamaa!

Tatizo la mtoto kushindwa au kuchelewa kutembea au kuongea lipo na huanza kuonekana hata baada ya kuzaliwa au baadae kulingana na visababishi vyake. Kitaalamu hujulikana kama cerebral palsy (CP).

Hali hii husababishwa na ubongo kukosa hewa (oxygen) kwa muda fulani hasa pale mtoto anapozaliwa akachelewa kulia. Pia wapo watoto wengine ambao hupata hiyo hali ukubwani hasa pale anapokabwa na kitu chochote kigumu kwenye njia ya hewa kwa muda (acquired CP) lakini kikatolewa kabla ya madhara mengine kama kifo kutokea. Ubongo ndio kiungo kinachosimamia na kuratibu utendaji kazi wa viungo vyote mwilini hivyo unapoathirika kwa kukosa hewa husababisha baadhi ya viungo vingine kuathirika mfano misuli kulea na kukosa nguvu.

Matibabu ya hali hii kwa ujumla ni mazoezi maalumu ambazo hutolewa na wataalamu wake (physiotherapist, speech therapist na occupational therapist) hospitalini. Mazoezi hayo husaidia viungo vya mwili kupata nguvu na kufanya kazi yake ya kawaida. Pia hujumuisha matumizi ya vifaa maalumu kama hizo walker na vingine.

Kwa hiyo pamoja na kumtafutia mwanao hicho kifaa ni vyema ukafika ktk hospital ambazo huduma hizo hutolewa na wataalamu husika kwani yatamsaidia sana mtoto pamoja na wewe mwenyewe.
Pole sana!.
 
Hili ni somo zuri sana.

Umejua kunipa Elimu.

Mtoto Yuko Geita - wapi anaweza kupata hii huduma kwa urahisi?

Maana hapo juu kuna mdau amesharudi CCBRT na Mhimbili.
 
Tafuta mtaalam wa tiba za asilo...hali hiyo huwapata watoto ambao wazazi wao hutoka nje ya ndoa...kwetu Tanga Kuna sawa mtoto anapewa ya kumkinga Ili hata mzazi akitoka akirudi jasho la huko aliko Toka lisimuathiri....!​
 
Hili ni somo zuri sana.

Umejua kunipa Elimu.

Mtoto Yuko Geita - wapi anaweza kupata hii huduma kwa urahisi?

Maana hapo juu kuna mdau amesharudi CCBRT na Mhimbili.
Kwa Geita nafikiri Bugando iko karibu, unaweza ukafika kuonana nao utasaidiwa na kama kuna haja ya kwenda CCBRT nafikiri watakuambia.
 
Naona nguvu anazo ila kuna shida za hapa na pale za kiafa. Ikiwemo kuongea hawezi ila anasikia na anaweza kuongea mambo anayojisikia.

Mpeleke mtoto hospitali, tafuta zile ambazo zina madaktari wenye taaluma ya milango ya fahamu/ubongo "Neurologist"
 
Back
Top Bottom