Aliekaa kihasarahasara ajitokeze
Salaam,
baada ya kukurupushwa na kiwatengu wakati natega ndoano ya kuvunja ndoa ya mimisa na Mwanathropolojia naomba kujitokeza kumzoa mwanamke yeyote ambae hajielewielewi au hajitambui ili nijiliwaze na kuponya majeraha ya kipigo nilichopata!
Sina masharti yeyote ili mradi tu awe amekaa kihasarahasara huku akiugulia maumivu mbalimbali ya mapenzi!
Naahidi kuishi nae kwa furaha kubwa na kwa upendo wa hali ya juu, hadi akina mimisa na kiwatengu washangae!
Naomba kuwasilisha,
Ahsanteni sana!
TheDealer
Huu ujio unashangaza na tena unaogopesha sijui kama utampata humu labda nenda majukwaa mengine waweza .pata huyo. MWANAMKE ALIYEKAAA KIHASARAHASARA!! sijui kama atatokea?
Baba umeingia choo cha kike nenda huko ulikotoka ndg
ONYO: Yani ni jinsi gani unavyotuona sisi wanawake ni hovyo sana hatuna mwelekeo wowote tuombe radhi mapema kabla hatujamwambia mtawala wa hapa CC.
njoo mango kinondoni ujipatie jinsia zakilebalari
Humu utawapata wapo wengi tu.
nimecheka sana aiseee....
Sasa Boss, wadai wataka li-mwanamke lolote! Na huna vigezo, ndy kusema hata asiye na marinda! We twende tu? Au?