Namuangalia Kobisi kwa mtazamo wa maumivu

Namuangalia Kobisi kwa mtazamo wa maumivu

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Kobisi ni muigizaji ambaye amejipatia umaarufu hivi karibuni mbali na kuwepo kwenye game kitambo. Tamthiliya ya kombolela imemfanya Kobisi aonekane na ajulikane. Kobisi ni kijana mkubwa mwenye mtoto mkubwa lakini hana msaada nyumbani kwa wazazi wake zaidi ya kuongeza mzigo kwa mzee wake.

Wakati Kobisi anapata umaarufu kama Rais wa Jobless Tanzania. Nawafikiria wakina Kobisi wakweli mtaani. Yaani mwanaume mwenye umri wa Kobisi uko nyumbani na dada zako halafu dada yenu mkubwa ndio anawapa kula. Nawaza ni kwa kiasi gani mwanaume asiyeweza kusaidia familia anavyoumia nafsini mwake kwa kuona hawezi kufanya vitu.

Mbali na kumuona Kobisi kuwa muigizaji tu, wako kina Kobisi wengi mtaani ambao kimsingi wanataka kufanya jambo ila mazingira hayawaruhusu
 
Kuna kipindi nilienda kuishi na bro wangu kiwalani maeneo ya bom bom. Aisee wanaume wa kule 95% wanabanana na dada zao au wazazi kwenye nyumba za familia/urithi. Wanaoa na kuzaliana nyumbani na hata ukipiga nao stori hawana mpango wa kuondoka makwao. Yaani nilikuwa dogolesi (fomfoo) lakini nilikuwa siwaelewi wanawaza nini asee.
 
Back
Top Bottom