Namuanzaje mamamkwe???

Namuanzaje mamamkwe???

Jaribu kuyashinda haya kwa kuwa mpole hasa ktk kipindi hiki ambacho wewe haupo karibu nae ukisharudi fanya uchunguzi wako kimya kimya naamini kuna utakalogundua. Ukilianzisha kwa sasa na ww uko mbali ni rahisi kupata hasara zaidi pia kuukosa ukweli wa huyo MCHUMBA WAKO.Kuwa na aman na tekeleza yaliyokupeleka huko then haya ya laki tano utayatatua ukiwa tayari NYUMBAN
 
Suala hapa ni uaminifu na sio ukubwa wa hela husika.

Ukicheka na nyani sasa huko mbeleni utavuna mabua, maana atasema aah jamaa hana tatizo hata nikikomba hela zake bila taarifa.
 
Usidai ila punguza mazoea na Mama mkwe asije akakufanya shamba la bibi ukishamuoa binti yake!
 
Suala hapa ni uaminifu na sio ukubwa wa hela husika.

Ukicheka na nyani sasa huko mbeleni utavuna mabua, maana atasema aah jamaa hana tatizo hata nikikomba hela zake bila taarifa.

Mkuu hapa na copy & paste,mawazo yako kama yangu.Issue sio laki tano.

Issue ni kile kitakacho jengeka hapa ukiinamisha kichwa chini,itakuja kukusumbua baadae,yaani mama mkwe asipate matatizo siku zote mpaka ulipo muachia mchumba ATM card?...Usiogope kumvimbia eti kwa vile unapenda,hata kama hatoweza kuzirudisha(kwa asilimia kubwa pesa katumia mchumba kwa kivulili cha Mama mkwe) basi weka clear kuwa hukupenda na asirudie tena.

Dai pesa yako mpaka wakome! Laki tano sio pesa ya kupeana ni ya kukopeshana aisee! Laki tano watu wanaweka mortgage kabisa! Uliya wajasiriamali watakuambia! Mtu anaweka bond TV, radio, simu na heleni za gold!
 
chakufanya hapo fanya mpango uchukue ATM YAKO NDIO MPANGO MZIMA. Mambo yakuuliza uliza mamamkwe yanaweza kukufanya ukose mke. Lol
 
wazazi wa mchumba wanamhusu nini wakati hata ndoa yenyewe bado. kila mtu abebe mzigo wako, ukipenda kuwasaidia sawa lakini si jukumu la huyu kaka.

pole mkuu namna ya kwenda kumwuliza mama mkwe mmmhhh pana ugumu.
Swali je wakati unamwambia atoe pesa kwa ajili ya wazazi/ndugu zako kuna kiasi chochote ulikuwa unampatia kwa ajili ya wazazi wake pia?
 
mimi naona tatizo umelianzisha wewe mwenyewe. iweje ATM card yakao umwachie mke mtarajiwa. watu wana ndoa na kila mtu ana ATM yake, wewe mwenzetu kulikoni? una uhakika hii itaendelea? maana usianzishe kitu halafu kiishie njiani. baadae ukafungua account nyingine ambayo hata mkeo haijui na hii ambayo yeye ana ATM usiweke pesa tena. huoni kama utakua umesababisha matatizo makubwa zaidi? kwa vile umelikoroga tangu mwanzo, linywe. kama ulivyosema mwenyewe pesa zina vishawishi, ndio hivi sasa. mama kapata short, mchumba mkwanja unatosha, kwanini nisimpe. unalalamika nini? si ndio matumizi ya pesa? ulitaka atumie ndio maana ukamwachia ATM card yako,matumizi yenyewe ndio kama haya.
 
Jielimishe kuhusiana na SIM Banking na faida.Ungekuwa unajua mapema ungejiunga na CRDB na matatizo hayo uliyonayo yasungekuwepo kabisa.POLE SANA
 
una uhakika gani kwamba mama mke alizichukua kweli?
 
Suala hapa ni uaminifu na sio ukubwa wa hela husika.

Ukicheka na nyani sasa huko mbeleni utavuna mabua, maana atasema aah jamaa hana tatizo hata nikikomba hela zake bila taarifa.

Mkuu hapa na copy & paste,mawazo yako kama yangu.Issue sio laki tano.

Issue ni kile kitakacho jengeka hapa ukiinamisha kichwa chini,itakuja kukusumbua baadae,yaani mama mkwe asipate matatizo siku zote mpaka ulipo muachia mchumba ATM card?...Usiogope kumvimbia eti kwa vile unapenda,hata kama hatoweza kuzirudisha(kwa asilimia kubwa pesa katumia mchumba kwa kivulili cha Mama mkwe) basi weka clear kuwa hukupenda na asirudie tena.

Mkuu anatakiwa kuchukua kadi yake kwa kigezo kwamba kwanini hakuambiwa wakati wanachukua?kwanini mpaka agundue mwenyewe.....hawa dada zetu bhana wanakosaga waume hivi hivi kwa uzembe,unakuta kanunulia hata laptop
 
Back
Top Bottom