Namuhurumia Samatta

Namuhurumia Samatta

laskaboza

Senior Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
142
Reaction score
1,584
Ki ukweli ndugu yetu huyu tunamtetea tu, lakini uwezo wake hauridhishi. Na sio mchezaji wa kwanza kutoka Genk kwenda EPL na kukutana na changamoto anazokutana nazo yeye.

Kuna mtu anaitwa Kevin De Bruyne alichukuliwa na Mourinho kutoka Genk akaenda Chelsea kwa ada ya Pound Mil 8, January 2012. Baadaye Mou akaona kama KDB uwezo wake mdogo akamtoa kwa mkopo kule Werder Bremen, Germany. Jamaa akakiwasha sana kule Germany mpaka Klopp (akiwa Dortmund) akataka kumchukua lakini Mou akamzuia kwenda, akamwambia bado ana mipango naye. Na alinukuliwa kocha wa Werder Bremen (Thomas Schaaf) akisema wangeshuka daraja kama sio juhudi binafsi za Kevin De Bruyne. Ilikua msimu wa 2012/2013.

Lakini KDB alivyorudi Chelsea akacheza game kama tatu tu halafu Mou akaanza kumpiga Bench tena karibu msimu mzima. KDB akaona isiwe tabu akamuomba Mou kwa huzuni sana kuliko aendelee kusugua Bench bora tu amuuze kule Bundesliga mazima maana anaona kama Chelsea haina mipango nae. Anaonekana kiwango chake ni duni.

Mou akaamua kumtupia Wolfburg kwa pound Mil 22, January 2014 kama garasha lililoshindwa kumridhisha. Lakini jamaa akaenda kukiwasha mbaya kabisa kule Bundesliga na kuchukua uchezaji bora huku akiweka assists record (2014/2015). Akiwa Wolfsburg, Offer zikamininika kutoka PSG, Bayern na Man City lakini yeye akaona kwa aina ya mpira anaocheza, Man City ndio itamfaa. Na August 2015, akauzwa kwenda Man City kwa kitita cha Pound Mil 76.

So, Chelsea walimuona hafai kama anavyoonekana Samatta Aston Villa. Lakini KDB hakukata tamaa mpaka leo hii ni miongoni mwa wacheza bora kabisa pale EPL. Na anakaribia kuvunja rekodi ya assists ya Thierry Henry. So samatta needs to deliver outstanding performance bila hivyo watamnyoa siku si nyingi.

Wazungu hawana huruma na mtu asiyeleta mabadiliko kwenye timu. Asijifariji kuwa sababu ya kutokufunga magoli ni kutokupewa pasi na na wachezaji wengine. Atatimuliwa asipojiongeza kujua namna bora ya kucheza epl na kupata matokeo. Kila la Kheri kwake. Akazane!

Ni mtazamo tu!
 
Samatta aongeze juhudi kwa kujituma zaidi, hope atakaa sawa tu na kuna hope ya Villa kubaki EPL baada ya kuifunga Arsenal,
Good luck SAMATTA.
 
Kimsingi uamuzi wa kuhamia Aston Villa ulikuwa haukuzingatia hadhari iliyokuwa mbele. Samatta bado ni mchezaju mzuri mwenye kiwango ila hajapatana na aina ya mchezo unaomfanya atambe.
 
Ki ukweli ndugu yetu huyu tunamtetea tu, lakini uwezo wake hauridhishi. Na sio mchezaji wa kwanza kutoka Genk kwenda EPL na kukutana na changamoto anazokutana nazo yeye.

Kuna mtu anaitwa Kevin De Bruyne alichukuliwa na Mourinho kutoka Genk akaenda Chelsea. Baadaye Mou akaona kama KDB uwezo wake mdogo akamtoa kwa mkopo kule Bremen, Germany. Jamaa akakiwasha sana kule Germany mpaka Klopp (akiwa Dortmund) akataka kumchukua lakini Mou akamzuia kwenda, akamwambia bado ana mipango naye. Na alinukuliwa kocha wa Bremen akisema wangeshuka daraja kama sio juhudi binafsi za Kevin De Bruyne.

Lakini KDB alivyorudi Chelsea akacheza game kama tatu tu halafu Mou akaanza kumpiga Bench tena. KDB akaona isiwe tabu akamuomba Mou kwa huzuni sana kuliko aendelee kusugua Bench bora amuuze kule Bremen mazima maana anaona kama Chelsea haimuhitaji kabisa. Anaonekana kiwango chake ni duni.

Mou akaamua kumtupia kule Bremen mazima kwa £ 20M kama garasha lililoshindwa kumridhisha. Jamaa akaenda kukiwasha mbaya kabisa kule Bremen na kuchukua uchezaji bora Bundesliga. Offer zikamininika kutoka PSG, Bayern na Man City lakini yeye akaona kwa aina ya mpira anaocheza, Man City ndio itamfaa.

So, Chelsea walimuona hafai kama anavyoonekana Samatta Aston Villa. Lakini KDB hakukata tamaa mpaka leo hii ni miongoni mwa wacheza bora kabisa pale EPL. Na anakaribia kuvunja rekodi ya assists ya Thierry Henry. So samatta needs to deliver outstanding performance bila hivyo watamnyoa siku si nyingi.

Wazungu hawana huruma na mtu asiyeleta mabadiliko kwenye timu. Watamtimua! Asijifariji kuwa sababu ya kutokufunga magoli ni kutokupewa pasi na na wachezaji wengine. Hii sababu ni ya kipuuzi kabisa. Kwani hao wachezaji wengine wanapataje mipira? Atatimuliwa asipojiongeza namna bora ya kutafuta matokeo. Kila la Kheri kwake.

Ni mtazamo tu!
We jamaa unachekesha.
Unamhurumia MTU mbaye mshahara wake wa wiki moja ni sawa na mshahara wa ukoo wenu miaka mitano
 
Kwanza De Bruyne hajacheza Bremen, hivyo hufuatilii mpira, kwa hiyo huna ruhusa ya kuuongelea
huyu jamaa anatulisha matango pori, De Bruyne alikuwa Wolfsburg na siyo Bremen.
 
huyu jamaa anatulisha matango pori, De Bruyne alikuwa Wolfsburg na siyo Bremen.

IMG_3532.JPG

Angalia katoka GENK kaenda Chelsea akaenda kwa Bremen then akauzwa wolfburg mazima ndio AISHA Chelsea
 
Utofauti wa samata na yikep nikwamba mmoja yuko England mwingene bongo
 
Kijana. You are very wrong. Alishawahi kuichezea Werder Bremen na picha yake hiyo hapo chini. So jifunze kufanya research kidogo kabla hujaonesha ujinga wako hadharani.

Una kingine usichokijua kuhusu mpira nikusaidie?View attachment 1513569
Mkuu ni kweli umepuyanga alitokea Wolfsburg ndio akaenda man city

Alafu bila aibu hutaki kurekebishwa
 
Kwanza De Bruyne hajacheza Bremen, hivyo hufuatilii mpira, kwa hiyo huna ruhusa ya kuuongelea
Aliichezea kwa loan fee baadae akaja kurudishwa Chelsea

Ndio akauzwa mazima kwa 22million pound kwenda kuitumikia Wolfsburg ya ujerumani.Akiwa huko alikiwasha kinoma
ndipo baadae akaja kuuzwa Manchester city na moto ukakolea.
 
Ki ukweli ndugu yetu huyu tunamtetea tu, lakini uwezo wake hauridhishi. Na sio mchezaji wa kwanza kutoka Genk kwenda EPL na kukutana na changamoto anazokutana nazo yeye.

Kuna mtu anaitwa Kevin De Bruyne alichukuliwa na Mourinho kutoka Genk akaenda Chelsea kwa ada ya Pound Mil 8, January 2012. Baadaye Mou akaona kama KDB uwezo wake mdogo akamtoa kwa mkopo kule Werder Bremen, Germany. Jamaa akakiwasha sana kule Germany mpaka Klopp (akiwa Dortmund) akataka kumchukua lakini Mou akamzuia kwenda, akamwambia bado ana mipango naye. Na alinukuliwa kocha wa Werder Bremen (Thomas Schaaf) akisema wangeshuka daraja kama sio juhudi binafsi za Kevin De Bruyne. Ilikua msimu wa 2012/2013.

Lakini KDB alivyorudi Chelsea akacheza game kama tatu tu halafu Mou akaanza kumpiga Bench tena karibu msimu mzima. KDB akaona isiwe tabu akamuomba Mou kwa huzuni sana kuliko aendelee kusugua Bench bora tu amuuze kule Bremen mazima maana anaona kama Chelsea haina mipango nae. Anaonekana kiwango chake ni duni.

Mou akaamua kumtupia kule Bremen mazima kwa pound Mil 22, January 2014 kama garasha lililoshindwa kumridhisha. Lakini jamaa akaenda kukiwasha mbaya kabisa kule Werder Bremen na kuchukua uchezaji bora Bundesliga na akaweka assists record. Akiwa Wolfsburg, Offer zikamininika kutoka PSG, Bayern na Man City lakini yeye akaona kwa aina ya mpira anaocheza, Man City ndio itamfaa. Na August 2015, akauzwa kwenda Man City kwa kitita cha Pound Mil 76, akitokea Wolfsburg.

So, Chelsea walimuona hafai kama anavyoonekana Samatta Aston Villa. Lakini KDB hakukata tamaa mpaka leo hii ni miongoni mwa wacheza bora kabisa pale EPL. Na anakaribia kuvunja rekodi ya assists ya Thierry Henry. So samatta needs to deliver outstanding performance bila hivyo watamnyoa siku si nyingi.

Wazungu hawana huruma na mtu asiyeleta mabadiliko kwenye timu. Asijifariji kuwa sababu ya kutokufunga magoli ni kutokupewa pasi na na wachezaji wengine. Atatimuliwa asipojiongeza kujua namna bora ya kucheza epl na kupata matokeo. Kila la Kheri kwake.

Ni mtazamo tu!
Nimesoma zaidi ya mara tatu.
Kwenye bandiko lako umekiri kutudanganya ya kuwa mou alimuuza dogo kwenda Bremen

Huku uhalisia ukiwa kuwa ni aliuzwa kwenda Wolfsburg.
 
Namungo wanammezea mate. Atawafaa kwa mechi za kimataifa.
 
Back
Top Bottom