Namungo FC 2-2 Simba SC | NBC Premier League | Ilulu Stadium

Namungo FC 2-2 Simba SC | NBC Premier League | Ilulu Stadium

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania NBC Premier League kupigwa leo ambapo Namungo FC anapepetana na Mnyama Mkali Mwituni Simba SC kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali hasa baada ya Namungo FC kuwa na rekodi mbaya ya kupoteza mchezo kila wanapokutana na Simba SC, pia wakiwa wamepoteza mchezo wao wa mwisho kwenye Premier League huku Simba SC akitoka sare ya bila kufungana na Watani wao wa Jadi.

Kocha wa Magolikipa wa Namungo FC amesema, Kuwa wao wamejiandaa vizuri, kiakili na kimwili kuhakikisha wanaiwakilisha vema nembo ya Namungo FC. Wanajua mchezo utakuwa mgumu, wanacheza na Simba SC ambayo imetoka kucheza michuano ya Kimataifa, na ina wachezaji wa Kimataifa lakini pamoja na yote haitawazua wao kukamilisha jambo lao la ushindi.

Kwa upande wa Kocha Pablo Franco amesema, mchezo utakuwa mgumu kwasababu hawajapata muda wa maandalizi, anaikumbuka vizuri Namungo FC kwenye michuano ya Mapinduzi aliwafunga 2-1 mchezo ulikuwa mgumu na ushindani mkubwa lakini wao Simba SC wanajitahidi kutafuta ushindi.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00 Jioni.. Usikose Ukaambiwa.

Kulitaka Mwana...Kulipewa Mwana

===============

00' Mpira umeanza uwanja wa Ilulu mkoani Lindi | Namungo FC 0-0 Simba SC.

07' Goooooooooooooaaal gooal

Namungo FC wanaandika bao la kwanza likifungwa na J Masawe kwa kichwa kufuatia mpira wa Kocha

Namungo FC 1-0 Simba SC.

11' Bandaaaa looo, shuti kali kutoka kwa Peter Banda, linachezwa na golikipa na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

14' Goooo laaaaaa hapanaaa ni Offside, Banda alikwamisha bao lakini Line 1 anasema mfungaji alikuwa ameotea, msako unaendelea

19' Almanusura Simba SC wapate bao, baada ya shuti kali la Bwalya kuchezwa na golikipa Kissu, ilikuwa nafasi nzuri Bwalya alishindwa kuchagua sehemu ya kufunga..!

23' Namungo wanamiliki mpira kwa sasa, huku wakijaribu kutafuta mpenyezo nyuma ya mabeki wa Simba.

27' Simba SC wanashambulia sasa, lakini Namungo FC wapo nyuma wote kulinda lango | Namungo FC 1-0 Simba SC.

31' Simba SC wanashambulia lango la Namungo, wachezaji Kagere, Banda, Kibu wanashindwa kufunga bao baada ya kutokea piga nikupige lango la Namungo.

35' Mpira ni 50 kwa 50 lakini Simba wamejitahidi sana kushambulia, lakini mashambulizi yao hayajazaa matunda.

42' Kapombe Goooooooooooooaaal gooal.

Shomari Kapombe anasawazishia Simba SC bao kwa shuti kali la pembeni na kumuacha golikipa Kissu akiruka bila mafaniko.

Namungo FC 1-1 Simba SC.

44' wakati huo huo Haruna Shamte yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha.

45+2' Kuendelea kuwa mapumziko kwenye Dimba la Ilulu, msako unaendelea

Emmanuel Charles anakwenda kurusha mpira lakini wanapoteza Namungo, wanachukua sasa Simba SC,

Naaam mpira ni mapumziko ambapo timu zote mbili zinakwenda mapumziko zikiwa na sare ya bao moja kwa moja.

HT; Namungo FC 1-1 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Ilulu mkoani Lindi Namungo FC na Simba SC.

Chirwa ameingia kuchukua nafasi ya Molinga upande wa Namungo FC.

53' Kukosa utulivu kunawakosesha Namungo FC kufunga bao.

54' Goooooooooooooaaal gooal..!

Chirwa anaipatia Namungo FC bao la pili kwa kichwa, mabeki wa Simba wakishindwa kuondoa hatari ile

Namungo FC 2-1 Simba SC.

Kombenisheni ya Chirwa na Lusajo, inabidi mabeki wa Simba wawe makini, kasi yao ni kali.

60' Simba wanafanya mabadiliko, ametoka Mzamiru na ameingia Sakho.

65' Sakho anajaribu kufungua ukuta wa Namungo FC, na kuachia shuti hafifu ambalo linadakwa na golikipa Kissu.

67' Hashim Manyanya anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi mchezaji wa Simba..!

69' Chirwa aliandika bao, lakini refa anakataa kwa madai kuwa Henock alichezewa madhambi kabla ya kufunga.. Wakati huo huo ameingia Bocco nafasi ya Banda.

75' Simba wanapata Free Kick, anapiga Kapombe anapiga ukuta wa mabeki wa Namungo FC, mpira unaokolewa.

77' Jacob Masawe anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumfokea mshika kibendera, wakati huo huo ameingia Ibrahim, akichukua nafasi ya Kichuya upande wa Namungo FC.

79' Kibu Goooooooooooooaaal gooal

Kibu Denis anasawazishia Simba SC bao kwa shuti la chini chini, baada ya piga nikupige.

Namungo FC 2-2 Simba SC.

Loooooooo, almanusura Namungo FC wapate bao la tatu kupitia kwa Lusajo, ilikuwa hatari, lakini Simba wanaokoa.

Simba wanajibu Counter mbele kuleee, Lakini Manyanya anakataa.

86' Simba SC wanafanya mabadiliko ametoka Onyango na Hussein, wameingia Wawa na Mhilu.

90+3' Kuendelea kumalizika kwa mchezo huu

Hatari lango la Simba SC, Chirwaaa, lakini unatolewa nje na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

Wanarusha Simba, unaokolewa tena, Kadi Nyekundu kwa Manyanya baada ya kupoteza muda, inapigwa kulee, anawahi Manula haraka haraka anaanza mbeleee,

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Namungo FC na Simba SC Wamegawana alama kwa kufungana mabao mawili kwa mawili.

FT: Namungo FC 2-2 Simba SC

... Ghazwat.....
 
Vikosi vyote vya Namungo FC na Simba SC
Screenshot_20220503-151042~2.jpg
Screenshot_20220503-151058~2.jpg
 
Chama , Sakho Mugalu out...

Anasema Mugalu ako na maumivu KWA kinena/groin ..

Sakho minor flu na other medical conditions zimamzuia kucheza leo
 
05' mpira umeanza kwa kasi uwanja wa Ilulu mkoani Lindi

Namungo FC 0-0 Simba SC

07' Goooooooooooooaaal gooal Namungo FC wanaandika bao la kwanza likifungwa na J Masawe kwa kichwa

Namungo FC 1-0 Simba SC
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom