Namungo FC ya Ruangwa-Lindi, yatinga ligi kuu

Joined
Mar 22, 2019
Posts
46
Reaction score
55
Na Bakari Chijumba

Timu ya Namungo Fc yenye maskani yake wilayani Ruangwa Mkoani Lindi ,imefanikiwa Kupanda daraja na kutinga Ligi kuu Tanzania Bara,baada ya kuichapa Mawenzi bao mbili kwa Moja,kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa ni miongoni mwa waliosafiri na timu hadi Morogoro ambapo amesema hawajaingia Ligi kushindana bali kwenda kushinda

Kocha Mkuu wa Namungo FC Hetmana Thierry amesema licha ya kutinga ligi kuu bado wana kiporo cha mechi mbili nyumbani .

"Kwanza tunamshukuru Mungu katujalia kuipandisha Timu,hilo lilikua ni lengo la uongozi..Pili bado ligi haijaisha sawasawa,Tumepanda(Ligi kuu) ila tuna mechi mbili za nyumbani,tukimaliza kuzicheza tutajipanga kwa ligi kuu" amesema Hetmana Thierry.
View attachment 1078537
 
Hii timu ina uwanja sio mbaya ila upo porini balaaa!! Bora wa mtibwa!
 
Wanadhani ligi kuu ni lelemama? Wajipange haswa! Kama wamepanda kwa hisani ya mtu basi wajipange kikwelikweli!
 
Nawashauri Mechi za nyumbani wachezee ilulu....hatoki mtu kule!!
 
hizi timu zinazopandishwa kisiasa hazijawahi kuwa na mafanikio
 
Nawashauri Mechi za nyumbani wachezee ilulu....hatoki mtu kule!!
Nimeimiss Kariakoo ya Lindi..
Kumbe mnawakumbuka hawa jamaa na Ilulu yao!!! Kuna siku nilitaka kushauri kila mechi ya Stars inayochezwa Tz, basi wakabidhiwe mikoba watu wa Lindi na kama vp mechi ziwe zinachezwa Ilulu 😀😀😀😀😀!! Bado namkumbuka Aden Rage alivyokuwa analilia kuhusu Kariakoo na uwanja wao baada ya Simba kutandikwa goli 3!

Nakumbuka kuna msimu karibu timu ZOTE ambazo zilienda Ilulu zilitandikwa kasoro Yanga ambao na wenyewe waliambulia sare!! Cha ajabu, huyo huyo ambae alitandika karibu timu zote nyumbani, hakupata hata point moja kwenye mechi za ugenini!!
 
Naona PM kajipandishia team yake!!! Soccer la bongo itaendelea kudumaa milele.
Inawezekana kajipindashia lakini tusisahau ile timu inapata support kubwa sana kutoka kwa wachimba madini na wafanyabiashara ay madini, bila kusahau mkoani na wilayani!

Kwa viwango vya timu zetu za daraja la kwanza, unaweza kusema Lyamungo ina kila kitu inachohitaji! Wakati timu zingine zinaweza kushindwa kufika eneo la tukio kutokana na kukosa usafiri, Lyamungo wana basi lake wenyewe!! Hata ukiwaona makocha wake, na wenyewe wana sifa… kwa mfano, kocha mkuu ni yule Mnyarwanda ambae alikuwa Biashara United akisaidiwa na Bakari Malima!!!

Zaidi ya hapo, hii timu originally ni ya "wana-Apollo" wa Lyamungo na mpaka kesho, wadhamini wake ni watu wanao-deal na madini!

So, kwa kuangalia viwango vya ukata wa timu zetu, unaweza kusema Lyamungo ni miongoni mwa timu chache zisizo na njaa… na hili ndilo muhimu zaidi kwenye soka!

Majaliwa aliingia kama wafanyavyo wanasiasa wote! Aliingia baada ya kuona Lyamungo imeshapata mafanikio ya kupanda daraja la kwanza ingawaje pia huwezi kupuuza umuhimu wake! Kwa mfano, tunajua daraja la kwanza limejaa magumashi kwa mechi za nyumbani! So, kv wengi wanaamini pale kuna mkono wa PM, basi wafanya magumashi wanaweza kuwa makini zaidi na magumashi yao wanapokutana na Lyamungo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…