Namungo wanaweza kuiadabisha Simba Jumatano, kaeni chonjo

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Mjumbe hauawi, nawajulisha viongozi wa Simba kuwa Namungo ikiwa na kocha msaidizi, beki wa zamani wa Yanga anayefanana sana na Karim Mandonga mtu kazi, Shadrack Nsajigwa maarufu kama Fuso ambaye katika maisha yake hatokuja kumsahau Emmanuel Okwi wako kwenye mikakati mizito ya kuikabili Simba yenye majeruhi kibao, mkitoa draw tu Yanga bingwa, nyie endeleeni kubishana huko.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
msimu huu yanga anachukua ligi mapema coz ana mipango mizizto ni kuleta kombe la afrika msimu huu huu,haina kungoja.Wazee wa robo tunawatikia kila la heri n atimu yenu unga mwana

Mkuu makombe ya Afrika yapo mengi. Ni vyema useme moja kwa moja kuwa kombe la shirikisho (a.k.a kombe la losers) ndio mna mipango nalo mizito. Hili kombe kila timu inaweza kushiriki.

NB: Unapotaja kombe la Afrika, kwetu sisi tunalitambua kombe moja tu ambalo ni la mabingwa (CAFCL). Huku timu chache sana hufanikiwa kushiriki.
 
Shirikisho, klabu bingwa yote makombe ya Afrika, ngoja yanga walete shirikisho hapa ndo tujue upo nae sawa na hizo robo fainali zako?
 
Na zamu hii watakuwa wanajipigia kama ngoma ya lizombe kwa litimu la kusumbuliwa na Ihefu mtajua hamjui
 
Mimi ninachofahamu kuna uwezekano mkubwa wa simba kudondosha pointi mpaka 7 hivi kwenye michezo yake 8 inayofuata baada ya ule waliocheza na Ihefu Fc, na kupata ushindi wa mbinde wa goli 1-0.

Na ndiyo kipindi hicho Mgosi mwenzangu Juma Mgunda atafungashiwa virago na kurudi zake Tanga.
 
Hongera yenu ninyi mliopata ushindi mnene wa goli 5-0 Jana Kwa Kagera sugar
 
una akili ndogo kwelikweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…