Namuona Muarabu Al Ahly akiombea Simba SC imfunge AS Vita Dar

Namuona Muarabu Al Ahly akiombea Simba SC imfunge AS Vita Dar

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Kwa hali inavyoendelea kundi la Simba, kama Al Ahly atashindwa kumfunga Vita Congo basi hatakuwa na njia nyingine zaidi ya kuomba kwa miungu wao Simba SC amfunge AS Vita kwa Mkapa ili angalau Ahly aweze kutinga robo fainali, hasa ukizingatia uwezo wa Simba wakiwa nyumbani.

Hii imekaa hivi, kama Simba atamfunga Msudan kwa Mkapa atafikisha pointi 10 (ushindi hii mechi ni wa muhimu sana), Ahly na Vita wakitoka suluhu Congo wote watakuwa na pointi 5 au kama Ahly ataruhusu kufungwa Congo atabaki na pointi zake 4 wakati Vita atafikisha pointi 7, mechi ya mwisho Vita anamaliza na msudan aliyemtandika 4-1 away, Vita atakuwa nyumbani.

Kwa hali hiyo, game ya Al Ahly Kinshasa ndio fainali yake, akikubali kufungwa amepotea, robo fainali wanaenda Simba SC na AS Vita Club, hapa lazima Al Ahly wapambane wawezavyo watoke na angalau pointi moja Kinshasa kwa usalama wao, vinginevyo wataaga mashindano katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.

CAF.PNG
 
Post yako ingechagizwa na msimamo wa ligi (table) ulivyo ingekua poa zaidi.
 
Post yako ingechagizwa na msimamo wa ligi (table) ulivyo ingekua poa zaidi.
Mkuu najaribu kuweka pale juu inagoma, tumia ya mdau hapo post no. 4.
 
Al Ahly sijui wana shida gani?
Nahisi labda Wachezaji hawamtaki kocha Msouth, wanataka mwarabu mwenzao au mzungu. So hata Kinshasa Ahly anaweza kufungwa au kusuluhu.
Kweli Mosimane anapigwa zengwe sana, hasa na wachezaji wa zamani wa Al Ahly, wale waarabu wanajidai wajuaji sana wakati wao kuifundisha hiyo timu hawawezi.
 
Ukiiangalia Al Ahly ya Sasa ni kama wachezaji wanajilazimisha kucheza.
Game ya jana wame draw kwa uzembe wao wenyewe, wamepoteza nafasi kibao, labda inaweza kuwa kuna figisu za chini hao wachezaji wanataka Mosimane aondoke, wanamchukua poa wakati akiwa na Mamelodi Mosimane aliwagonga 5 walipokutana.
 
Huyo As Vita hawezi kuwa na GD ya nne...maana alipata goli nne dhidi ya Al mereikh na goli mbili dhidi ya Al ahly jumla sita...pia amefungwa goli moja na Simba,moja na Al mereikh na mbili na Al ahly jumla goli nne ukitoa unapata mbili...so GD2 ndo inatakiwa ionekane hapo kwa As Vita...kuna makosa.
 
Yes wamekosea GD za VITA CLUB
 
Mashindano bado, kuna point 9 za second round zinashindaniwa, simba akikosa point ametupwa nje.
 
Uko sahihi,
Screenshot_20210307-081208.png
 
Huyo As Vita hawezi kuwa na GD ya nne...maana alipata goli nne dhidi ya Al mereikh na goli mbili dhidi ya Al ahly jumla sita...pia amefungwa goli moja na Simba,moja na Al mereikh na mbili na Al ahly jumla goli nne ukitoa unapata mbili...so GD2 ndo inatakiwa ionekane hapo kwa As Vita...kuna makosa.
Nazan kuna makosa yamefanyika as vita na al harly GD ni 2
 
Simba alikosea kutomfunga Msudani.

Vita na Al Ahly wanaweza songa mbele endapo mechi ijayo tukashindwa pata matokeo.

Kwa sasa tumuombee AS Vita ampige Mwarabu afu tumfunge Msudani

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
 
Mashindano bado, kuna point 9 za second round zinashindaniwa, simba akikosa point ametupwa nje.
Simba next round hamna hamna hakosi Point 4, yaan afungwe Cairo, a draw na Vita Kisha amchape Msudan. Atakua na total 11 points jumla.

Waliobaki watahitaji points 7 kufikia hizo 11 za Simba. Yaan washinde mbili na draw moja. Katika hizo mbili za kushinda kila mmoja atavuna point 3 kwa Msudan.

Itabaki points 4. Vita akidraw na Simba atahitaji kumchapa Ahly pale Kinshasa. Na Ahly endapo atamfunga Simba Cairo na Msudan atahitajika kufanya kazi ya ziada Kinshasa.

So atakaeshinda Lubumbashi ndo atakaepita na Simba endapo atafanikiwa kupata Point 4 mzunguko wa pili.
 
Simba next round hamna hamna hakosi Point 4, yaan afungwe Cairo, a draw na Vita Kisha amchape Msudan. Atakua na total 11 points jumla...
Ni kweli lakini lazima simba ifanye homework
 
Back
Top Bottom